YANGA YAPATA MWALIKO KENYA
YANGA YAPATA MWALIKO KENYA
Gavana wa Kaunti ya Siaya nchini Kenya, James Orengo amewasilisha mwaliko rasmi kwenda klabu ya Young kwaajili ya kushiriki ufunguzi wa uwanja wa Siaya tarehe 01 January 2025.
Mwaliko huo uliwasilishwa kwa Rais wa Klabu hiyo, Injinia Hersi Said ambaye mwishoni mwa wiki alikuwa nchini Kenya kushiriki Kikao cha Kamati ya Utendaji cha Shirikisho la soka barani Afrika (CAF)
Yanga inatarajiwa kuchuana na mabingwa wa Kenya, Gor Mahia katika mchezo wa ufunguzi wa uwanja huo.
