Yanga yaifuata Simba KMC Complex
Yanga yaifuata Simba KMC Complex
Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuwajulisha Wanachama, Mashabiki pamoja na Umma kwa ujumla kuwa, utautumia Uwanja wa KMC Complex kama Uwanja wake wa Nyumbani kwa mechi zote za Ligi Kuu ya NBC zilizosalia msimu huu wa 2024/2025.
Hivyo hivyo, Young Africans Sports Club itautumia uwanja wa KMC Complex kama uwanja wake wa nyumbani kwenye mechi za Kombe la Shirikisho la CRDB na michezo mingine ya nyumbani ambayo kanuni itaruhusu kuutumia uwanja huo.

Yanga yaifuata Simba KMC Complex
Awali Yanga walikuwa wanatumia uwanja wa Azam Complex uliopo Chamanzi kama uwanja wake wa nyumbani hadi mchezo wao wa mwisho dhidi ya Tabora United ambapo and walipoteza kwa goli 3 kwa 1.
Kwa sasa Yanga itaungana na watani wake wa jadi Simba SC na KMC FC ambao wanautumia uwanja wa KMC Complex kama uwanja wao wa nyumbani.

Yanga yaifuata Simba KMC Complex
