YANGA Kuifuata TP Mazembe Alhamisi
YANGA Kuifuata TP Mazembe Alhamisi
Baada ya kurejea nchini salama, Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka Jijini Dar es salaam Alhamisi ya tarehe 12 kuelekea Jijini Lubumbashi nchini DR Congo kwaajili ya mchezo wa raundi ya tatu Ligi ya Mabingwa dhidi ya TP Mazembe.
Mchezo huo wa Kundi A unatarajiwa kupigwa Jumamosi ya Disemba 14,2024 Kuanzia Saa 10:00 jioni.
Utakuwa mchezo mgumu kwani TP Mazembe wanahitaji kushinda ili kuwa na nafasi ya kufuzu robo Fainali sawa na Young Africans ambao pia mchezo huo ni muhimu kwao.
Jisajili na 1Win ushindi ni 100% Bofya HAPA, hakikisha umeweka Promo Code ambayo ni A19B ili kupata bonus ya Kujisajili ya asilimia 200 sawa na kiwango chako Cha Kwanza.
Katika Msimamo wa Kundi A TP Mazembe wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 1 waliyoipata dhidi ya MC Alger ya Algeria hapo hapo Lubumbashi.
Kwa upande wa Young Africans wao hawana pointi yoyote baada ya kupoteza michezo yote miwili ya awali dhidi ya Al Hilal Omdurman nyumbani na MC Alger ugenini.
Kutokana na matokeo hayo Wachezaji wa Young Africans wanapaswa kufahamu kuwa wanakwenda Lubumbashi kucheza mechi ya jasho na damu.
