Klabu ya Young Africans inatarajiwa kuondoka nchini kesho Alhamisi asubuhi, kuelekea Ethiopia tayari kwa mchezo wa mkondo wa kwanza raundi ya pili michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika CAF Champions League 2024/2025 dhidi ya CBE ya Libya.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumamosi ya September 14 katika uwanja wa Abebe Bikila, kuanzia saa 9:00 Alasiri.
Kuelekea safari hiyo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa jambo jema kwao haitakuwa safari ndefu kwani itawachukua takribani saa 3 kutoka Dar es salaam hadi Addis Ababa
Aidha nyota 14 waliokuwa katika majukumu ya timu za Taifa wamekamilisha majukumu yao jana na baadhi wanatarajiwa kuungana na timu moja kwa moja huko Ethiopia.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Post Views: 75