WEZESHA Portal Mfumo mpya wa utoaji Mikopo asilimia 10
WEZESHA Portal Mfumo mpya wa utoaji mikopo asilimia 10, Mikopo ya halmashauri online,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kuwa, Serikali imeamua mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu iliyokuwa imesitishwa hapo awali imerejeshwa kwa majaribio kuanzia mwezi Julai 2024 katika Halmashauri 10 hapa Nchini kwa mfumo mpya wa usimamizi.
Waziri Mchengerwa amezitaja Halmashauri zote 10 zitakazokuwa za majaribio hapa Nchini ni Halmashauri ya Majiji ya Dar es salaam na Dodoma, Manispaa za Kigoma Ujiji na Songea, Halmashauri za miji ni Newala na Mbulu pamoja na Halmashauri za Wilaya ya SIHA, Nkasi, Itilima na Bumbuli.
Utaratibu ulioboreshwa unahusisha uanzishwaji wa Kitengo cha Usimamizi wa utoaji wa mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa Kamati ya usimamizi wa utoaji wa mikopo katika ngazi za Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Halmashauri na Kata.
Mhe.Waziri Mchengerwa amesema kuwa, miongoni mwa majukumu ya Kamati ngazi ya Kata ni pamoja na kutambua waombaji, kuthibitisha vikundi vya mikopo na kuvisajili katika mfumo mpya unaitwa Wezesha Portal na baada ya usajili Kamati itawasilisha ngazi ya Wilaya kwa hatua zaidi.
Uboreshaji wa mfumo huu mpya wa utoaji wa mikopo kwa Vikundi vya Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu utaondoa changamoto mbalimbali zilizokuwa hapo awali kabla ya zoezi la utoaji wa mikopo kusimamishwa mwezi Aprili,2023.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: WEZESHA Portal Mfumo mpya wa utoaji Mikopo asilimia 10