Wasiochukua Vitambulisho Kufungiwa NIDA zao

Wasiochukua Vitambulisho Kufungiwa NIDA zao
Wasiochukua Vitambulisho Kufungiwa NIDA zao
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imetangaza kusitisha matumizi ya namba za utambulisho kwa wale waliokaidi kuchukua vitambulisho vyao.
Tangazo hilo linakuja ikiwa zimesalia siku 15 kufikia ukomo wa agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, la kusambaza vitambulisho milioni 1.2 vilivyotengenezwa na mamlaka hiyo, ambapo vitambulisho hivyo bado havijachukuliwa na wenyewe.
FAHAMU Kitambulisho Chako Cha NIDA Kilipo
Januari 13, 2025, akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari, Waziri Bashungwa alieleza kuwa tangu atoe agizo hilo, vitambulisho 400,000 kati ya vile vilivyokuwa vimekaa ofisini kwa muda mrefu vilitolewa kwa wananchi.
Kwa mujibu wa barua iliyotolewa na NIDA leo Ijumaa ya January 17, 2025 na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo James Kaji, imeeleza wale wote ambao hawajajitokeza kuchukua vitambulisho vyao na watakaopokea ujumbe mfupi wa maandishi katika simu zao, wanatakiwa kufika katika ofisi za NIDA za wilaya walizojiandikisha kuchukua vitambulisho vyao.
“Watakaoshindwa kufanya hivyo, matumizi ya namba yao ya utambulisho wa taifa (NIN) yatasitishwa baada ya mwezi mmoja tangu kupokea ujumbe huo,” imeeleza barua hiyo.

Wasiochukua Vitambulisho Kufungiwa NIDA zao

Nimetafuta kituo nilichochukulia sijapata