Waliofariki Kuporomoka kwa Ghorofa la Kariakoo Wafikia 20

Filed in Habari by on 20/11/2024 0 Comments

Waliofariki Kuporomoka kwa Ghorofa la Kariakoo Wafikia 20Waliofariki Kuporomoka kwa Ghorofa la Kariakoo Wafikia 20

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefika Kariakoo Jijini Dar es salaam leo Novemba 20,2024 muda mfupi baada ya kurejea kutoka Brazil, ambapo amekagua shughuli za uokoaji na kisha kuongea na Wananchi ambapo pamoja na mambo mengine amesema hadi kufikia asubuhi leo Watu 20 wamefariki kutokana na maafa ya ghorofa kuporomoka.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA
Waliofariki Kuporomoka kwa Ghorofa la Kariakoo Wafikia 20

Waliofariki Kuporomoka kwa Ghorofa la Kariakoo Wafikia 20

Rais Samia amesema “Jitihada zetu kubwa katika tukio hili imekuwa kuwaokoa wenzetu walionasa katika jengo lile wakiwa hai lakini kama tunavyoambiwa jitihada haziondoshi kudra ya Mungu, pamoja na jitihada tulizofanya kuna wenzetu tumewapoteza”

Waliofariki Kuporomoka kwa Ghorofa la Kariakoo Wafikia 20

Waliofariki Kuporomoka kwa Ghorofa la Kariakoo Wafikia 20

“Taarifa niliyopewa leo kwamba mpaka saa tatu asubuhi tumepoteza wenzetu 20 ambao Serikali imeshirikiana na Familia kuwasitiri wenzetu”

“Hili sio pigo kwa Familia zilizopoteza Watu wao pekee yao ni pigo letu kama Watanzania na tunaguswa pia, ni kumbukumbu ya kutisha kwa wenzetu waliookoka hapa, kwa jinsi jengo lilivyo Mtu akitoka hai bila shaka hawapo sawa (kisaikolojia), niombe wasifadhaike, wajipe moyo na tuendelee na shughuli zetu za kawaida bado Mungu ana kazi nao”

Katika hatua nyingine, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewajulia hali na kuwapa pole majeruhi wa ajali hiyo ambao wamelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Ilala Jijini Dar es Salaam.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!