Waliofariki Kuporomoka kwa Ghorofa la Kariakoo Wafikia 13
Waliofariki Kuporomoka kwa Ghorofa la Kariakoo Wafikia 13
Watu 13 wamethibitika kufariki Dunia na wengine 84 kujeruhiwa kufuatia ajali ya kuporomoka kwa jengo katika eneo la Kariakoo mkoani Dar es Salaam, iliyotokea jana Novemba 16, 2024.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa idadi hiyo ya vifo pamoja na majeruhi ni ya hadi saa nne asubuhi leo Novemba 17, 2024.
Rais Samia ametoa idadi hiyo alipokuwa akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kuporomoka kwa moja kwa jengo hilo la ghorofa Kariakoo .
Ametoa salamu hizo leo Novemba 17, 2024, Jijini Rio de Janeiro nchini Brazil ambapo yupo kwaajili ya kushiriki mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Kundi la G20 unaotarajiwa kuanza kesho Novemba 18, 2024.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: Waliofariki Kuporomoka kwa Ghorofa la Kariakoo Wafikia 13