VIINGILIO Yanga vs Al Hilal Sudan 26 November 2024
VIINGILIO Yanga vs Al Hilal Sudan 26 November 2024
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Young Africans, ametangaza Viingilio vya mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Hilal ya Sudan ambao utapigwa November 26 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 10:00 jioni.
Viingilio hivo ni Kama ifuatavyo; VIP A itakuwa ni Tsh 30,000, VIP B itakuwa Tsh 20,000, VIP C itakuwa Tsh 10,000 na Viti vya rangi Machungwa pamoja na Mzunguuko itakuwa ni Tsh 3,000.
Aidha Mauzo ya tiketi hizo yameanza leo kupitia mitandao ya simu na vituo mbalimbali vitakavyotajwa leo hii.
Ally Kamwe amewataka Mashabiki na Wanachama wa Young Africans kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ili kuipa hamasa timu yao.
Kamwe amesema kuwa haijawahi kutokea Yanga ikapoteza mechi tatu mfululizo katika mashindano tofauti.
Hii ni mechi ya kila Mwananchi kujitokeza kuongeza nguvu katika kuhakikisha ushindi unapatikana.
