VIINGILIO Simba vs CS Sfaxien 15 December 2024

Filed in Michezo by on 11/12/2024

VIINGILIO Simba vs CS Sfaxien 15 December 2024VIINGILIO Simba vs CS Sfaxien 15 December 2024

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba SC, Ahmed Ali ametangaza Viingilio vya mchezo wa tatu wa hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Ili kuhakikisha Wanasimba wengi wanajitokeza uwanja wa Benjamin Mkapa kuishangilia timu yao, Ahmed amesema kuwa uongozi umepunguza bei ya viingilio ambapo kwa Mzunguuko kiingilio kitakuwa Tsh 3,000 tu.

Kwa Tanzanite itakuwa Tsh 250,000, Platinum itakuwa Tsh 150,000, na VIP A itakuwa Tsh 30,000, VIP B Tsh 20,000, VIP C Tsh 10,000 na Kwa Viti vya rangi ya Machungwa itakuwa Tsh 5,000.

Pata bonus ya asilimia 200 Ukijiunga na 1Win Bofya HAPA Kujisajili, hakikisha umeweka Promo Code ambayo ni A19B ili kupata bonus ya Kujisajili.

Aidha Ahmed amesema kuwa lengo ni kuhakikisha wanakwenda kujaza uwanja wa Benjamin Mkapa na kuipa hamasa Simba katika mchezo ambao alama tatu lazima zibaki nyumbani.

“Tarehe 15 siku ya Jumapili saa 10:00 jioni kunako Uwanja wa Mkapa ni siku ya kumuangamiza CS Sfaxien. Na hili halitawezekana kwa Fadlu peke yake, kwa Camara peke yake bali kwa Wanasimba wote kuja uwanjani, hakuna Mwanasimba anayetakiwa kubaki nyumbani. Kama kweli tuna nia ya kumuangamiza mpinzani wetu basi hatuna budi aache nyumba yake aje Benjamin Mkapa.”

“Kila kiongozi wa tawi, kila kiongozi wa kundi ana jukumu la kuhimiza Wanasimba wenzake kuja uwanjani. Hakuna sababu yoyote ya Mwanasimba kubaki nyumbani. Utaipendaje Simba kama huifati ilipo?”

“Kupoteza na CS Constantine kusitutoe kwenye reli, nafasi yetu ya kwenda robo fainali bado nyeupe kabisa. Nafasi yetu bado iko wazi tukifanya vizuri mechi inayofata.”

“Baada ya kupoteza mchezo wa juzi kuna wenzetu wakaanza kukata tamaa lakini niwambie tu tuko salama sana, hakuna kilichobadilika, nafasi yetu ya kwenda robo fainali iko palepale. Niwakumbushe msimu juzi mpaka mchezo wa pili hatukuwa na alama yoyote na tukaibukia kwa Vipers na kila mmoja anakumbuka Mnyama akavuka kwenda robo fainali.”

“Mchezo wa Jumapili lazima kila Mwanasimba ajue umuhimu wake maana mpinzani tunayekutana nae anataka kufufukia kwetu na sisi hatuko tayari kuona CS Sfaxien anafufukia kwetu. Hakuna ambaye amewahi kupata uhai ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa.”

“Kwa kuwa mechi hii tunataka tuwe na mashabiki wengi Benjamin Mkapa, tunataka kujaza Benjamin Mkapa. Mara ya mwisho kujaza Uwanja wa Mkapa ilikuwa ni Simba Day. Tumeamua kuweka viingilio ambavyo havitampa mtu sababu ya kutokuja uwanjani lakini pia tupo karibu na sikukuu za mwaka. Na sisi tumeamua kupunguza viingilio ili kila Mwanasimba aje uwanjani,” alisema Ahmed Ally.

VIINGILIO Simba vs CS Sfaxien 15 December 2024

VIINGILIO Simba vs CS Sfaxien 15 December 2024


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Comments are closed.

error: Content is protected !!