VIGEZO vya kuwa Wakala wa NBC Bank

Filed in Makala by on 08/12/2024

VIGEZO vya kuwa Wakala wa NBC BankVIGEZO vya kuwa Wakala wa NBC Bank,Kupitia Mashine za POS za NBC, unaweza kupokea malipo ya bidhaa na huduma zako kutoka kwa mteja wako yeyote mwenye kadi ya VISA.

Hii inakupunguzia kazi ya kuhesabu fedha taslimu na hatari ya kuzitunza kwenye eneo lako la biashara hadi utakapopeleka benki.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Je Biashara yako itanufaikaje?

  • Ni njia rahisi na nzuri zaidi kwa wamiliki wa kadi za VISA kulipia bidhaa na huduma mbalimbali
  • Inasaidia kulipia kwa haraka na kwa usalama zaidi
  • Itapunguza upotevu wa fedha kwenye duka lako
  • Itapunguza kuwa na fedha taslimu kwenye biashara
  • Inasaidia kumalizana na malipo kwa haraka – inapunguza foleni na wateja kuwa na furaha
  • Inapunguza safari za benki kwenda kuweka fedha taslimu
  • Inakuthibitishia kukamilika kwa malipo mara moja
  • Unakuwa na uhakika wa malipo kwa miamala yote iliyothibitishwa
  • Inakusaidia kuhakiki kadi ya uongo na iliyofungiwa kwa haraka sana
  • Inakutayarishia ripoti na majumuisho ya mauzo kwenye taarifa ya akaunti yako.

Nani anaweza kuwa na Mashine hizi?

Wafanyabiashara ikiwemo:

  • Makampuni yaliyosajiliwa
  • Wabia wabiashara
  • Wamiliki wa Biashara

Vipi kuhusu uhalifu?

Sera ya NBC ya Kuzuia Uhalifu inaelekeza kuwapatia taarifa zote muhimu wafanyabiashara wenye mashine za POS za NBC ili kujiepusha na uhalifu.

Halikadhalika, NBC inafuata Kanuni zote za EMV tangu Agosti 2008.

Kuwa wakala wa NBC unapaswa kukidhi vigezo vifuatavyo.

  • Uwe na leseni ya biashara.
  • Uwe na TIN.
  • Uwe na shs 200,000 kwaajili ya kulipia mashine ya uwakala.
  • Kitambulisho chako kimojawapo kati ya cha NIDA, cha Mpiga Kura, Leseni ya Udereva ama pasi ya kusafiria.
    6.Barua ya utambulisho wa makazi toka serikali ya mtaa.

Ninapeleka maombi wapi?

Wafanyabiashara wenye sifa wanaweza kutuma maombi kupitia kwa Meneja Mahusiano wa NBC, tawi lolote la NBC au kwenye ofisi za NBC.

Mawasiliano:

Idara ya Huduma za Wafanyabiashara
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Mtaa wa Sokoine /Azikiwe
Makao Makuu, Ghorofa ya Kwanza
Dar es Salaam

Fax: +255 22 2112367


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Comments are closed.

error: Content is protected !!