Dereva wa bodaboda ambaye hujapata mafunzo rasmi ya udereva, huu ni wakati wako! kujifunza kwa gharama nafuu.
VETA inakupa fursa ya kipekee ya kupata mafunzo ya udereva wa pikipiki kwa ada iliyopunguzwa kutoka Shilingi 120,000 hadi Shilingi 30,000 tu! Ni punguzo la kipekee la asilimia 75%.
UTAJIFUNZA: Usalama Barabarani na Matumizi ya Vifaa Kinga Udhibiti wa Mwendo na Matengenezo ya kawaida ya Pikipiki Uendeshaji wa Dharura na Mbinu za Kukabiliana na Ajali
Sheria za Udereva na Usalama wa Abiria Usimamizi wa Kifedha na Ujasiriamali.
VYETI RASMI VYA UDEREVA
Baada ya kukamilisha mafunzo, utatunukiwa cheti rasmi cha udereva kutoka VETA.
Cheti hiki kitakutambulisha kuwa una uwezo wa kuendesha pikipiki kwa ustadi na usalama.
MIKOA INAYOHUSIKA
Awamu ya kwanza ya mafunzo haya inafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Manyara, Tabora, Shinyanga, Simiyu, Tanga, Arusha, na
Kilimanjaro.
LINI MAFUNZO YATAANZA
Mafunzo yataanza rasmi tarehe 20 Oktoba 2024 katika vyuo mbalimbali vya VETA.
KUJIUNGA
Fika kwenye chuo cha VETA kilicho karibu nawe uchukue fomu.
Unaweza pia kutembelea tovuti yetu
www.veta.go.tz au piga simu 0755 26 74 89 kwa maelezo zaidi.