Utaratibu wa Malipo HESBL 2024/2025
Utaratibu wa Malipo HESBL 2024/2025, Malipo ya Gharama za Chakula na Malazi, Vitabu na Viandikwa, Mahitaji Maalumu ya Kitivo, Mafunzo kwa Vitendo na Gharama za Utafiti zitalipwa moja kwa moja kwa mwanafunzi;
Wakati Ada ya Mafunzo italipwa moja kwa moja kwenye taasisi husika ya Elimu ya juu.
Malipo yote yatafanyika baada ya mnufaika kuthibitisha kwa njia itakayokuwa imeelekezwa na Taasisi husika ya Elimu ya juu kupitia akaunti za Benki zilizohakikiwa, ambazo ziliwasilishwa wakati wa kuomba Mkopo.
Ikitokea Mwanafunzi hajasaini kwa wakati, mkopo utarejeshwa HESLB baada ya siku 30 kutoka tarehe ambayo taarifa ilifikishwa chuoni na mnufaika kutaarifiwa kuhusu malipo hayo kupitia simu yake ya mkononi.
Kiasi Kilichorejeshwa hakitalipwa tena kwa mwanafunzi na hakitakuwa sehemu ya deni lake.
Aidha malipo yoyote yatakayofuata lazima athibitishwe na Chuo.
JINSI YA KUREJESHA MKOPO
Baada ya kuhitimu Masomo ya Elimu ya Juu, mnufaika wa mkopo atatakiwa
kurejesha mkopo wake wote kwa makato yasiyopungua asilimia kumi na
tano (15%) ya mshahara wake wa kila mwezi au kiwango kisichopungua TZS
100,000.00 kwa mwezi kwa mnufaika aliye kwenye sekta isiyo rasmi.
Iwapo mnufaika ataachishwa/atakatisha masomo, mkopo huo wote utalipwa kwa
mkupuo. Mikopo yote inatozwa asilimia moja (1%) ya ada ya uendeshaji kwenye
deni la msingi la mnufaika kwa mara moja.
