USAJILI Uliokamilika dirisha dogo la Usajili 2024/2025
USAJILI Uliokamilika dirisha dogo la Usajili 2024/2025
Nijuze Habari inakuelea orodha ya sajili zilizokamilika Katika dirisha hili dogo la usajili Msimu wa 2024/2025.
Dirisha hilo lilifunguliwa tarehe 15 December 2024 na limefungwa tarehe 15 January 2025.
Klabu ya Singida Black Stars imekamilisha usajili wa Golikipa, Amas Obasogie kutoka Bendel Insurance FC ya nchini kwao Nigeria.
Klabu ya Dodoma Jiji FC imekamilisha usajili wa beki, Abdi Banda kama mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba na Baroka FC ya Afrika Kusini.
Klabu ya Tabora United imekamilisha usajili Mshambuliaji mzawa, Emmanuel Mwanengo Kutoka Vakhsh Bokhtar ya Tajikistan.
Klabu ya Mashujaa FC imekamilisha usajili wa beki wa kushoto, Yahya Mbegu Kwa Mkopo hadi mwisho wa msimu Kutoka Singida Black Stars.
Mashujaa FC pia imekamilisha usajili wa Mshambuliaji Danny Lyanga Kutoka JKT Tanzania FC.
Klabu ya Pamba Jiji FC imekamilisha usajili wa Mshambuliaji Mathew Tegis kutoka Shabana ya nchini Kenya.
Klabu ya Pamba Jiji imekamilisha usajili wa golikipa wa timu ya Taifa ya Sierra Leone, Mohamed Nbalie kwa mkopo Kutoka Singida Black stars.
Pamba Jiji pia imekamilisha usajili wa Mshambuliaji, Francois Bakari raia wa Cameroon.
Klabu ya Singida Black Stars imekamilisha usajili wa aliyekuwa Kiungo mshambuliaji, Serge Pokou mwenye umri wa miaka miaka 24 Kutoka Al Hilal Omdurman SC ya Sudan.
Klabu ya Young Africans imekamilisha usajili wa winga, Jonathan Ikangalombo mwenye umri wa miaka 22 Kutoka AS Vita Club ya kwao DR Congo.
Klabu ya Tabora United imekamilisha usajili wa Kiungo wa ulinzi ‘Cedric Martial Zemba’ raia wa Cameroon mwenye umri wa miaka 25 kutoka Klabu ya Soka ya Tourga ya nchini Morocco.
Klabu ya KenGold FC imekamilisha usajili wa beki wa zamani , Steven Duah Namungo FC na Kagera Sugar Duah.
Klabu hiyo pia imekamilisha usajili wa Kiungo Mshambuliaji wa zamani wa Vilabu vya Simba na Yanga, Benard Morrison Kwa mkataba wa miezi sita.
Klabu ya Namungo FC imekamilisha usajili wa Mshambuliaji, Saleh Karabaka Kwa Mkopo wa miezi sita Kutoka Simba SC
Klabu ya Singida Black Stars imekamilisha usajili wa, beki Frank Kwabena Assinki raia wa Ghana mwenye umri wa miaka 22 kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka HB Køge ya Denmark ambayo ilimtoa kwa mkopo KFUM Roskilde tangu mwaka 2021.
Klabu ya KenGold FC imekamilisha usajili wa Kiungo Mshambuliaji, Lassa Gradi Kiala raia wa DR Congo mwenye umri wa miaka 26 Kwa mkataba wa miezi sita Kutoka Zanaco FC.
Beki Israel Patrick Mwenda amejiunga na Young Africans kutoka Singida Black Stars Kwa Mkopo wa miezi sita.
Kiungo Mshambuliaji, Deus David Kaseke amejiunga na Pamba Jiji FC ya Mwanza kama Mchezaji huru.
Beki Sandale Komanje amejiunga na Ken Gold akitokea Tabora United FC ya Mkoani Tabora.
Emmanuel Mwanengo amejiunga na Tabora United ya Tabora kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Mwanengo amejiunga na Tabora United kama mchezaji huru baada ya mkataba wake na Vakhsh ya nchini Tajikistan kumalizika.
Hamadi Majimengi amejiunga na Pamba Jiji kwa mkopo wa miezi sita Kutoka Singida Black Stars.
Klabu ya Namungo FC, imefanikiwa kumrejesha aliyewahi kuwa beki wao Derick Mkombozi raia wa Burundi.
Mshambuliaji, Habibu Hajii Kyombo amejiunga na klabu ya Pamba Jiji ya Jijini Mwanza.
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Yanga Yusuf Athumani amejiunga na klabu ya Fountain Gate kwa mkataba wa mwaka mmoja kama mchezaji huru.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: USAJILI Uliokamilika dirisha dogo la Usajili 2024/2025