UFAHAMU Ugonjwa wa Marburg na Jinsi ya Kujikinga

UFAHAMU Ugonjwa wa Marburg na Jinsi ya Kujikinga
UFAHAMU Ugonjwa wa Marburg na Jinsi ya Kujikinga
FAHAMU JINSI UGONJWA WA MARBURG UNAVYOENEA
Marburg ni Ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Marburg na unaambukizwa kwa haraka.
Ugonjwa huu unaenea kwa njia zifuatazo;
Kugusa Majimaji ya mwili kama vile;
- Kinyesi
- Matapishi
- Damu
- Mkojo na
- Jasho
Kugusa vitu vilivyotumiwa na mtu mwenye ugonjwa wa Marburg mfano;
- Vyombo
- Magodoro na Matandiko pamoja na
- Nguo

UFAHAMU Ugonjwa wa Marburg na Jinsi ya Kujikinga

Dalili za Ugonjwa wa Marburg
JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA MARBURG
Epuka kugusa majimaji ya mwili wa mtu mwenye dalili za Ugonjwa wa Marburg mfano damu, mate, matapishi, jasho, mkojo au na kinyesi
Epuka kugusa au kuosha maiti ya mtu aliyefariki kutokana na Ugonjwa wa Marburg, toa taarifa kwa wataalam wa afya ili mazishi yafanyike kwa kufuata taratibu za afya na utu
Epuka kugusana na mtu mwingine mfano kusalimiana kwa kupeana mikono, kukumbatiana au kubusiana
Nawa mikono kwa maji tiririka na sabuni mara kwa mara
Epuka kula au kugusa mizoga au wanyama mfano popo, nyani, tumbili au swala wa msituni
Wahi au muwahishe mtu mwenye dalili za Ugonjwa huu katika kituo cha kutolea huduma za afya ili kuepuka kueneza maambukizi katika jamii
Serikali ya Tanzania imejipanga kuhakikisha inaendelea kutoa huduma bora, sahihi na kwa wakati, hivyo endapo utaona mtu mwenye mojawapo ya dalili zilizotajwa toa taarifa haraka katika kituo cha huduma za afya kilicho karibu, ofisi ya serikali ya kijiji/mtaa/ kata au piga simu 199 bila malipo.

JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA MARBURG
