Tigo yabadilisha jina Sasa ni Yas, yataja sababu

Filed in Habari by on 27/11/2024 0 Comments

Tigo yabadilisha jina Sasa ni Yas, yataja sababu Tigo yabadilisha jina Sasa ni Yas, yataja sababu

Chapa ya Kampuni ya huduma za simu chini Tanzania Tigo Tanzania imebadilishwa na sasa itakujulikana kwaa jina la Yas.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Kampuni hiyo ambayo wakati inaingia nchini miongo mitatu iliyopita ilianza kwa jina la Mobitel Mwaka 1994 kabla ya kuitwa Buzz Mwaka 2004 na Tigo Mwaka 2026 imetambulisha jina hilo jipya Novemba 26, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Tigo yabadilisha jina Sasa ni Yas, yataja sababu

Tigo yabadilisha jina Sasa ni Yas, yataja sababu

Mbali ya kubadilika chapa ya kampuni, jina la huduma zake za miamala ambazo awali zilijulikana kwa jina la Tigo Pesa limebadilika na sasa litaitwa Mixx by yas.

Yas (zamani Tigo) inamilikiwa na kampuni ya Honora Tanzania Public Limited ambayo ni sehemu ya kampuni mama ya Axian Telecom Group.

Katika uzinduzi wa jina jipya, imeelezwa ni hatua muhimu ya kuonyesha dhamira ya kuongoza katika ubunifu wa kidijitali na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi Tanzania nzima.

Kubadilishwa majina ya Tigo na Tigo Pesa hakujafanyika Tanzania pekee bali ni mpango wa Kampuni ya Axian Telecom Group kuwa na jina moja katika kampuni zake tanzu zote barani Afrika, ili kuwa na chapa ya kiuanamajumui yenye nguvu Afrika.

Nchi zingine zaidi ya Tanzania ni Togo, Madagascar, Senegal na Comoro.

Tigo yabadilisha jina Sasa ni Yas, yataja sababu

Tigo yabadilisha jina Sasa ni Yas, yataja sababu

Kuhusu mabadiliko hayo, Mwenyekiti wa Bodi wa kampuni hiyo, Rostam Aziz amesema kuwa: “Mabadiliko haya ni ishara ya dhamira ya kuendelea kuwekeza na kuendeleza mabadiliko ya kidijitali Tanzania Bara na Visiwani. Kwa pamoja na Axian Telecom Group tupo tayari kuendelea kufungua fursa mpya, kuhamasisha ubunifu, kujenga kesho iliyo bora na kuunganisha watu zaidi.”

Amesema Yas na Mixx by Yas zinadhamiria kubeba maono ya kampuni ya kuwa kiungo muhimu cha ubunifu wa kidijitali barani Afrika kwa kutengeneza fursa zisizo na kikomo, kuboresha maisha kupitia huduma za kidijitali na huduma za kifedha kwa mamilioni ya Watanzania.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Axian Telecom, Hassanein Hiridjee amesema kuwa: “Kampuni imekuwa kwenye safari thabiti ya kuunganisha Waafrika kupitia chapa zao zinazokua. Kuweza kuwezesha kizazi kijacho hatuna budi kuwa na chapa inayotoa huduma katika mataifa tofauti na chapa hii inaiunganisha Afrika.”

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa mpito wa Kampuni ya Honora Tanzania, Jerome Albou amesema kuwa mabadiliko ya chapa ni mpango wa kampuni mama wa zaidi ya miaka miwili iliyopita na yamefanyika katika nchi tano ambazo wanatoa huduma.

“Tumekuwa tukiongoza katika ubunifu, tutaendelea kufanya hivyo, watu watarajie mambo mazuri. Kila siku tunaangalia mteja anataka nini nasi tunaboresha zaidi na zaidi,” amesema.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags: ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!