TCU Majina 9890 ya Waliochaguliwa Chuo zaidi ya Kimoja awamu ya tatu 2024/2025, Majina ya waliochaguliwa chuo zaidi ya kimoja awamu ya tatu PDF.
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inaufahamisha umma, Taasisi za Elimu
ya Juu na wadau wa Elimu ya Juu ndani na nje ya nchi kuwa udahili katika awamu ya Tatu na ya mwisho kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa mwaka wa masomo 2024/2025
umekamilika.
Majina ya waliodahiliwa katika Awamu ya Tatu yametangazwa na vyuo husika.
WAOMBAJI WALIODAHILIWA KATIKA CHUO ZAIDI YA KIMOJA
Waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika awamu ya tatu na
wale ambao hawakuweza kuthibitisha udahili katika awamu zilizopita,
wanapaswa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia leo
tarehe 19 hadi 21 Oktoba, 2024.
Uthibitisho huo unafanyika kwa kutumia
namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za
simu au barua pepe (email) walizotumia wakati wa kuomba udahili.
Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika.
Aidha, uthibitisho wa udahili ufanyike kupitia akaunti ambayo muombaji
alitumia wakati wa kuomba udahili.
Kwa urahisi wa rejea, orodha ya majina
ya waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja inapatikana kwenye tovuti ya
WITO KWA WAOMBAJI UDAHILI
Waombaji udahili wa Shahada ya Kwanza wanakumbushwa kuwa masuala
yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika chuo kimoja yawasilishwe
moja kwa moja kwenye vyuo husika.
Kwa wale ambao watapata changamoto
katika kujithibitisha, vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na
kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu
zilizowekwa.
Orodha ya waombaji waliodahiliwa zaidi ya Chuo kimoja au Program zaidi ya moja katika awamu ya tatu ya udahili na wale ambao hawakuthibitisha awamu zilizopita kwa mwaka wa masomo 2024/2025 imeambatanishwa kwenye PDF hapa chini;
MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Post Views: 93