JINSI ya Kupata Leseni Online Kupitia Mfumo wa Tausi

Filed in Makala by on 10/09/2024 0 Comments
JINSI ya Kupata Leseni Online Kupitia Mfumo wa TausiJINSI ya Kupata Leseni Online Kupitia Mfumo wa Tausi
Ingia kwenye Kivinjari (Browser) katika
kompyuta yako na kisha andika anuani
ifuatayo https://tausi.tamisemi.go.tz
JINSI YA KUJISAJILI KATIKA MFUMO WA TAUSI
Mfumo una njia kuu mbili za kujisajili
hivyo mtumijiaji atachagua njia moja
wapo.
1.Njia ya kutumia maswali, njia hii ya
kwanza itakutaka kujibu kwa usahihi
maswali yanayo husiana na taarifa
zako za NIDA na endapo utafanikiwa
kujibu kwa usahihi mfumo utakupokea.
2.Njia ya kutumia nywila mahususi
(OTP), Nywila hii hupatikana baada ya
mtumiaji mpya kungiza namba yake ya
NIDA na namba ya simu iliyotumika
kwenye NIDA na kuomba OTP.
KUJISAJILI KWA KUHAKIKI MASWALI YA NIDA.
KUJISAJILI KWA KUHAKIKI MASWALI YA NIDA.
Njia hii ya kujisajili kwa kutumia
maswali mbalimbali yahusuyo taarifa
zako za NIDA.
  • Chagua chaguo la kwanza wakati
    wa usajili.
  • Ingiza namba yako ya NIDA kwa
    ufasaha kisha bonyeza kitufe cha
    search
  • Baada ya kuchagua itakupasa
    kujibu maswali yote yahusuyo
    NIDA kwa usahihi
  • Baada ya hapo mfumo utakupokea.
Bofya kitufe kilichooandikwa Continue
ili kuweza kuendelea katika kipengele cha maswali.
Anza kujibu maswali kwa ufasaha
kama mfumo utakavyokuwa unakuhitaji
NB: ENDAPO UTAFANIKIWA KIJIBU
MASWALI YOTE KWA UFASAHA, MFUMO UTAKURUHUSU KUJISAJILI NA UTAPATA UJUMBE WA KUFANIKIWA.
KUJISAJILI KWA KUTUMIA OTP
Njia hii ya kujisajili kwa kutumia Nywila
mahususi (OTP)
  • Chagua chaguo la pili wakati wa usajili.
  • Baada ya kuchagua itakupasa kuingiza namba yako ya NIDA kwenye box la kwanza na namba yako ya simu ambayo umesajili kwa kutumia namba yako ya NIDA kwenye box la pili.
  • Baada ya hapo bofya kitufe kilichooandikwa Request OTP.

Njia hii ya kujisajili kwa kutumia Nywila
mahususi (OTP).

  • Ingiza namba yako ya NIDA (NIN) kisha
  • Subiri na utapokea ujumbe mfupi wa maandishi (sms) kutoka namba 15200 kupitia namba yako ya simu iliyosajiliwa na NIDA yako
  • Ingiza namba sita ulizopokea kwenye viboksi katika menyu ya usajili.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA
  • Ingiza barua pepe yako(Email) kwa
    usahihi katika box namba moja.
  • Ingiza namba yako ya simu
    kwa usahihi katika box namba mbili.
  • Tengeneza Nywila(Password)
    ambayo utakuwa unaitumia katika
    kuingia katika mfumo wa mapato (TAUSI).

KUNGIA KWENYE MFUMO BAADA YA KUJISAJILI

Kwa waliokwisha kujisajili katika mfumo
wa TAUSI.

Fuata hatua zifuatazo:-

  • Hakikisha kifaa chako kimeunganishwa na intaneti
  • Ingia katika kivinjari (Browser)
  • Andika anuani ya mfumo https://tausi.tamisemi.go.tz
  • Kisha bofya neno Ingia “Sign In”
KUINGIZA TAARIFA ZA TIN KATIKA MFUMO
Bonyeza alama za nukta tatu zilizopo
upande wa juu kulia, kisha bonyeza Wasifu wangu “My profile” halafu bonyeza maneno INDIVIDUAL TIN DETAILS.
Baada ya kubonyeza maneno INDIVIDUAL TIN DETAILS, bonyeza neno Update Now na kisha soma masharti ya matumizi ya TIN na hakikisha umeweka
alama ya vema kuashiria kwamba
umeyaridhia.
Baada ya kuridhia vigezo na masharti ya matumizi ya TIN, bonyeza neno na kisha mfumo wa TAUSI utawasiliana na mfumo wa TIN kuthibitisha TIN uliyoiandika.
NB: Ikiwa leseni ya biashara inayoombwa kupitia mfumo ni ya
kampuni, kampuni itaandika
barua ya kumtambulisha mwakilishi wake ambaye namba yake ya
NIDA itatumika kwa ajili ya usajili pamoja na kufanya maombi ya leseni husika.
Bonyeza neno Update Now na kisha ingiza namba za mlipa kodi “TIN” yako halafu bonyeza neno Search.
JINSI YA KUOMBA LESENI YA BIASHARA MTANDAONI
Gusa alama za mistari minne iliyozungushiwa duara kuweza
kuona mpangilio wa kodi mbalimbali katika mfumo.
Ili kuanza kuomba Leseni, Bofya
kitufe kilichoandikwa Application.
Chagua Business License kisha bofya Apply Now.
Fuata malekezo ya kuchagua Mkoa na Halmashauri ambayo unaombea Leseni yako kisha bonyeza NEXT.
Fuata malekezo ya kuchagua Mkoa na
Halmashauri ambayo unaombea leseni yako kisha bonyeza NEXT.
Chagua majibu ya maswali kuhusu ikiwa umewahi kushtakiwa pamoja na uraia, kisha Bofya Next->
Kwa ufasaha jaza jina la biashara
endapo ni kampuni au jina la biashara
lililosajiliwa rasmi.
Kama hamna rudia majina yako kama yanavyoonekana katika TIN
  • Chagua kundi kuu la biashara
  • Chagua aina ya biashara
  • Chagua muda wa leseni unayoomba
    (mfano mwaka, miaka 2, miaka 3)
  • Andika namba ya TAX CLEARANCE
  • Chagua Kata ambapo biashara yako
    itakuwepo
  • Chagua Mtaa
  • Andika Block number
  • Andika Plot number
  • Kisha, bonyeza Next->
Mfano wa muonekano wa taarifa
za biashara zilizojazwa.
Kwa kila aina ya biashara mfumo utakutaka kupakia viambatanisho mbalimbali, hakikisha unakuwa na viambatanisho hivyo katika mfumo wa kielektoniki lazima viwe katika fomati ya PDF ili uweze kuvipakia kwenye mfumo
NB: Ukubwa wa viambatanisho usizidi 2 MB.
Baada ya kujaza taarifa za biashara na
eneo unaloenda kufanyia biashara yako
  • Pakia nyaraka mbalimbali kadri
    zinavyohitajika katika mfumo kwa
    kubofya neno Choose.
  • Ukisha bofya tafuta eneo katika kifaa chako ambapo viambatanisho
    umeviweka kisha pakia nyaraka moja baada ya nyingine.

NB: Hakikisha nyaraka zako zinakuwa
katika fomati ya PDF.

Baada ya kupakia viambatanisho
hivyo:

  • Mfumo utakuonyesha muda na
    tarehe ambapo viambatanisho vimepakiwa
  • Mfumo utakupa.nafasi ya
    kuondoa kiambatanisho kama umekosea kwa ku Delete
  • Kama taarifa zote zipo sahihi
    bofya Next->

Hakiki taaarifa zako zote
katika vipengele vifuatavyo:-

  • Application Details
  • Principal Business Information
  • Business Contact
  • License Issuing Authority
  • Kama taarifa zote zipo sahihi bofya kitufe cha SAVE ili kuweza kutuma
    taarifa zako Halmashauri kwa hatua zinazofuata.

Hakiki taaarifa zako zote katika vipengele vifauatavyo:-

  • Application Details
  • Principal Business Information
  • Business Contact
  • License Issuing Authority

Kama taarifa zote zipo sahihi bofya kitufe cha SAVE ili kuweza kutuma taarifa zako Halmashauri kwa hatua zinazofuata.

Baada ya kuwasilisha maombi yako Maafisa watayaona maombi yako
na kufanya mambo yafuatayo:

  • Ukaguzi wa nyaraka kama zipo sahihi
  • Kuangalia usahihi katika ujazwaji wa fomu yako
  • Baada ya kila kitu kukamilika na kukubaliwa, mfumo utakupa
    kumbukumbu ya malipo “Control number” na utalipia kisha utachapisha “Print” leseni yako katika mfumo.

JINSI YA KUPAKUA LESENI YA BIASHARA

Bonyeza neno Leseni ya Biashara ili uweze kupakua “Download” leseni yako.

Bonyeza nukta tatu chini ya neno Actions, kisha bonyeza neno Print License kupakua leseni yako.JINSI ya Kupata Leseni Online Kupitia Mfumo wa Tausi


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!