TANZIA: Mwigizaji Fredy Kiluswa Afariki Dunia
TANZIA: Mwigizaji Fredy Kiluswa Afariki Dunia
Muigizaji wa tamthilia na Filamu Nchini, Fredy Kiluswa amefariki Dunia Leo Jumamosi tarehe 16 November 2024 wakati akipatiwa matibabu Hospitalini.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa baadhi ya wasanii wakiwemo Jacob Steven (JB) na Steve Mengele maarufu Steve Nyerere.

TANZIA: Muigizaji Fredy Kiluswa Afariki Dunia
Fredy ametamba na filamu na tamthilia mbalimbali ikiwemo tamthilia ya Mzani wa Mapenzi inayoonyeshwa katika channel ya Sinema Zetu ya Azam TV.
JB amesema kuwa “Ni kweli nimepigiwa simu amefariki, nilikuwa nina taarifa kwamba jana alikuwa Muhimbili na baadaye akapelekwa Mloganzila, presha ilikuwa haishuki na sasa hivi nimepigiwa amefariki, tulimchangia kwaajili ya matibabu, alikuwa na tatizo la moyo na baadaye akawa anapata dawa na moyo wake ulikuwa unaenda vizuri lakini baadaye presha ikapanda akaanguka akapelekwa Muhimbili, presha haikushuka tena ndio amefariki, alikuwa anaumwa”
Nijuze Habari tunatoa pole Kwa Familia na tasnia ya Sanaa Kwa kumpoteza mpendwa wetu Fredy.
