TANZIA: Dkt. Faustine Ndugulile Afariki Dunia

Filed in Habari by on 27/11/2024 1 Comment

TANZIA: Dkt. Faustine Ndugulile Afariki DuniaTANZIA: Dkt. Faustine Ndugulile Afariki Dunia

Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson kwa masikitiko makubwa ametangaza kifo cha Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile kilichotokea usiku wa kuamkia leo November 27, 2024 Nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Dkt. Tulia amesema “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile, kwa niaba ya Wabunge natoa pole kwa Familia, Wakazi wa Kigamboni na Watanzania wote, Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi”

“Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelela kutolewa, Bwana ametoa na Bwana ametwaa, apumzike kwa amani”

TANZIA: Dkt. Faustine Ndugulile Afariki Dunia

TANZIA: Dkt. Faustine Ndugulile Afariki Dunia


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Comments (1)

Trackback URL | Comments RSS Feed

  1. Walter Nyirenda says:

    May his soul rest in peace

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!