TANGAZO la Zabuni ya Maghala SIFACU 2025

TANGAZO la Zabuni ya Maghala SIFACU 2025
TANGAZO la Zabuni ya Maghala SIFACU 2025
1. Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima Mkoa wa Singida (SIFACU Ltd) kinatangaza zabuni ya utunzaji wa ghala kwa ajili ya msimu wa 2025/2026.
2. Kwa idhini ya Bodi ya Chama Kikuu, Mwenyekiti wa Bodi anatangaza zabuni shindani ya Kitaifa (National Competitive Tendering) kwa zabuni ya Utunzaji na uendeshaji wa Maghala kama ifuatavyo:-
MAHITAJI YA ZABUNI

MAHITAJI YA ZABUNI
3. Mzabuni mmoja anaruhusiwa kuomba ghala zaidi ya moja endapo atakuwa endapo atathibitisha kuwa na uwezo.
4. Mchakato wa Zabuni hii utafanyika kwa njia shindani ya Kitaifa (National Competitive Tendering) kwa mujibu wa Mwongozo wa Ununuzi na Ugavi wa vyama vya Ushirika Tanzania Bara na Sheria na kanuni za ununuzi wa Umma na ni zabuni ya wazi kwa wazabuni wote wenye sifa zinazohitajika.
5. Kitabu cha Zabuni kinapatikana baada ya kulipia ada ya Zabuni kwa gharama ya Fedha za Kitanzania Shilingi Milioni Moja na laki tano tu (1,500,000.00) ambazo hazitarudishwa.
Fedha zote zilipwe kwenye Akaunti ya chama KIKUU CHA USHIRIKA CHA WAKULIMA MKOA WA SINGIDA (SIFACU) Nambari 50810084633 Singida Farmers’ Co-operative Union Limited, Benki ya NMB.
6. Waombaji wawasilishe zabuni zao (Nakala mbili), nakala halisi moja na kopi moja zikiwa zimefungwa kwenye bahasha kwa umakini na kutiwa lakiri na kuainisha Zabuni namba na Mahitaji kwa zabuni aliyoomba juu ya bahasha ya maombi yake.
7. Muda wa kutuma maombi ya Zabuni ni Siku 6 baada ya Tangazo kutolewa, kuanzia tarehe 20 Januari, 2025 hadi tarehe 25 Januari, 2025 Saa Nane kamili mchana (8:00) na SIKU HIYO NDIO UFUNGUZI.
8. Zabuni zitakazochelewa hazitafanyiwa kazi wakati wa tathmini ya zabuni bila kujali sababu zozote za kuchelewa kwao.
9. Bahasha ziandikwe Namba ya Zabuni na sio jina la chama au Jina la Mzabuni.
SIFA ZA JUMLA ZA MUOMBAJI
1. Waombaji wenye nia ya kushiriki, wanakaribishwa Ofisi ya SIFACU SINGIDA
2. Muombaji awe na akaunti benki itakayowezesha kufanya malipo kwa njia ya hundi.
3. Cheti cha Usajili wa Kampuni/Kikundi;
4. Cheti cha usajili wa Mamlaka mbalimbali za Usajili za Serikali.
5. Leseni halali ya Biashara;
6. Hati Safi ya Mlipa kodi (Tax Clearance Certificate);
7. Orodha ya mikataba iliyotekelezwa karibuni inayojumuisha majina na anuani za Wanunuzi kwa ajili ya uthibitisho (Uzoefu wa kazi husika).
8. Tamko la Dhamana ya Zabuni;
9. Hati ya Kiapo cha Nguvu ya Kisheria Iliyoidhinishwa.
10. Fomu ya Uadilifu iliyo katika kitabu cha Zabuni
11. Nyaraka nyingine muhimu zitaazohitajika kwenye zabuni.
