TAARIFA ya Waziri Simbachawene Kuhusu Usaili na Ajira Za Walimu 2025

TAARIFA ya Waziri Simbachawene Kuhusu Usaili na Ajira Za Walimu 2025
TAARIFA ya Waziri Simbachawene Kuhusu Usaili na Ajira Za Walimu 2025
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene leo amezungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, na kutangaza kuwa kuanzia tarehe 14 Januari hadi terehe 24 Februari, 2025, usaili wa kada za Ualimu utaendeshwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa kushirikiana na;
- Ofisi ya Rais (UTUMISHI)
- Ofisi ya Rais (TAMISEMI)
- Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
- Wizara ya Afya
- Tume ya Utumishi wa Walimu
- Ofisi za Wakuu wa Mikoa yote na wataalamu mbalimbali kutoka katika Taasisi za Umma.
Aidha Usaili huo una lengo la kujaza nafasi elfu kumi na nne mia sita na arobaini na nane (14,648) zilizotolewa na Mheshimiwa Rais kwa lengo la kupunguza uhaba wa walimu nchini.
Waziri Simbachawene amewasihi sana wale wote walioitwa kwenye usaili wajiandae vyema kwa usaili huo kwani nafasi hizi ni za ushindani.
Vilevile, kulingana na mahitaji ya elimu kwa sasa, Waziri Simbachawene amesema kuwa wataajiriwa wataalamu wa fani za Amali.
Hivyo, anawasihi sana wale wote watakaopata nafasi ya kuajiriwa, wawe tayari kujiendeleza ili kuweza kukidhi matakwa ya ajira zao katika Utumishi wa Umma.
Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa usaili huo wa kada za Ualimu utafanyika katika Mkoa ambao kila msailiwa anaishi.
Lengo kuu la utaratibu huu ni kuwapunguzia gharama za kusafiri na mambo mengine wasailiwa wote.
RATIBA YA USAILI AJIRA WALIMU
Hiyo ni kutokana na tangazo la kumtaka kila msailiwa kuhuisha taarifa zake katika akaunti yake ya Ajira Portal sehemu iliyoandikwa ‘current physical adress’ kwani ndipo wasailiwa wamepangiwa vituo vya usaili kulingana na anuani walizojaza.
Aidha Mhe. Simbachawene amesema kuwa Usaili wa awali wa kuandika (Mchujo) kwa kada za Ualimu utafanyika kwa njia ya kuandika kwa mkono kwa kada zote na ngazi zote za elimu.
Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene amewakumbusha wote watakaokwenda kwenye usaili wahakikishe wanabeba vyeti vyao Halisi kikiwemo Cheti cha Taaluma na Cheti cha kuzaliwa.
Vilevile, wasailiwa wanapaswa kuja na namba zao za usaili walizotumiwa kwenye akaunti zao za ajira portal pamoja na kuzingatia Ratiba kama ilivyopangwa na Sekretarieti ya Ajira
UNAWEZA KUANGALIA LIVE TAARIFA HIYO HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: TAARIFA ya Waziri Simbachawene Kuhusu Usaili na Ajira Za Walimu 2025