SIMBA yapiga hodi Uhamiaji Kuombea Uraia Wachezaji Wake

SIMBA yapiga hodi Uhamiaji Kuombea Uraia Wachezaji Wake
SIMBA yapiga hodi Uhamiaji Kuombea Uraia Wachezaji Wake
Klabu ya Simba SC Tanzania imeandika barua kwa Kamishina Jenerali wa Uhamiaji nchini ikiwaombea uraia wa Tanzania wachezaji wake 9 Kati ya 12 ambao imewasijili kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu ya Bara.
Kupitia Barua iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Mrutaza Mangungu imesema kuwa;
Kwa mujibu wa kanuni za usajili za TFF, Klabu ya Ligi kuu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni 12 katika msimu mmoja wa ligi.
Simba Sports Club ina wachezaji wa kigeni ambao wamekua na mchango mkubwa katika maendeleo ya Klabu kimpira na kutoa uwakilishi mzuri kimataifa.
Hata hivyo, wachezaji hao wamekua wakikosa nafasi katika nchi zao hususan timu za taifa.
Kwa kuzingatia mahitaji ya Klabu na Mchango wa wachezaji hao, Simba Sports Club inaomba wachezaji tisa (9) wa kigeni waweze kupatiwa uraia wa Tanzania, ili waweze kufanya kazi kama watanzania.
Sababu ya maombi haya ni kwamba wachezaji hao bado ni vijana hivyo wana muda mrefu wa kutumika Tanzania.
Zaidi, wanaweza kuwa chachu ya maendeleo ya Mpira wa miguu Tanzania.
Tunaomba pia wakati wa mchakato huu, wachezaji hao ambao orodha yao imeambatanishwa wahesabike kama Watanzania na kuondoshewa malipo yote yanayotakiwa kufanywa kwa mchezaji wa kigeni.
Kwa barua hii, tunaomba ofisi yako iridhie maombi yetu na kutupa taratibu husika ili kukamilisha mchakato.
Ni imani yetu kuwa ombi hili litashughulikiwa ipasavyo kutokana na maamuzi ya Serikali kuruhusu mchakato wa aina hiyo kufanyika.

SIMBA yapiga hodi Uhamiaji Kuombea Uraia Wachezaji Wake

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: SIMBA yapiga hodi Uhamiaji Kuombea Uraia Wachezaji Wake