SIMBA Yalaani Vitendo Vilivyofanywa na Viongozi wa Pamba Jiji
SIMBA Yalaani Vitendo Vilivyofanywa na Viongozi wa Pamba Jiji
Uongozi wa klabu ya Simba umesikitishwa na vitendo visivyo vya kiungwana vilivyofanywa na viongozi wa timu ya Pamba Jiji FC, kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda kwa kutumia Askari Polisi mkoani humo.
Kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu ya NBC, Simba tulipaswa kutumia Uwanja wa CCM Kirumba kufanya mazozezi ya mwisho kuelekea mchezo wetu wa kesho Novemba 22,2024 dhidi ya Pamba lakini hali isiyokuwa ya kawaida maafisa wa timu hiyo waligoma kutoka Uwanjani.

SIMBA Yalaani Vitendo Vilivyofanywa na Viongozi wa Pamba Jiji
Pamoja na jitihada zote za kuwasihi, kupisha mazoezi lakini viongozi wa Pamba hawakukubali na kuendelea kusalia Uwanjani wakijifungia katika chumba cha Mikutano.
Muda mfupi baadae mazoezi yakiwa yanaendelea, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mheshimiwa, Mtanda akiambatana na Maafisa wa Polisi waliokuwa na vyeo mbalimbali huku wengine wakiwa na silaha walifika uwanjani hapo na kuingia ndani ya uwanja bila maelezo ya msingi wanakwenda kufanya nini.
Baada ya timu kumaliza mazoezi na kutaka kuondoka uwanjani, gari ya Polisi lilizuia msafara wa wachezaji na makocha huku wakiwakamata na kuwapandisha kwenye gari lao Meneja wa timu, Patrick Rweyemamu na Kocha Msaidizi, Selemani Matola ambao waliwaachia baada ya mabishano.

SIMBA Yalaani Vitendo Vilivyofanywa na Viongozi wa Pamba Jiji
Klabu hiyo imesema kuwa inalaani matumizi ya nguvu yaliyotumika katika sakata hili na kuwakamata maafisa wa klabu yetu bila ya sababu za msingi kwani jambo hilo linaonekana kama jitihada za kudhoofisha timu yetu kuelekea mchezo wa kesho.
Baadae Rweyemamu na Matola waliachiwa na msafara kurejea hotelini.
Simba tunalaani vitendo vya matumizi ya dola katika mpira wa miguu, na tunawakumbusha viongozi wenye Mamlaka kutumia mamlaka yao katika njia sahihi.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: SIMBA Yalaani Vitendo Vilivyofanywa na Viongozi wa Pamba Jiji