SIFA za Kujiunga na Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI)

Filed in Education by on 20/01/2025 0 Comments
SIFA za Kujiunga na Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI)

SIFA za Kujiunga na Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI)

SIFA za Kujiunga na Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI)

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA
Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo kilichopo Dodoma ni taasisi ya elimu inayotoa mafunzo mbalimbali kwa lengo la kuimarisha ujuzi na maarifa katika usimamizi wa serikali za mitaa na maendeleo ya jamii.
Chuo hiki kinatoa kozi mbalimbali zinazolenga kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa umma na sekta binafsi.
Namna ya Kuomba Kujiunga na Masomo Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI)
  • Astashahada (NTA Level 4 – Basic Technician Certificate)
Sifa za Kujiunga na Masomo Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI) 
Sifa za kujiunga na kozi mbalimbali katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo zinatofautiana kulingana na ngazi ya kozi.
Ngazi ya Cheti (NTA Level 4)
Sifa za Kujiunga:
  • Kidato cha Nne (Form Four) na ufaulu wa angalau daraja la nne (Division IV).
Ngazi ya Diploma (NTA Level 5)
Sifa za Kujiunga:
  • Mwombaji awe amepata angalau ufaulu wa “Principal Pass” moja na “Subsidiary” katika mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) AU awe na Astashahada (NTA Level 4 Basic Technician Certificate) toka Chuo chochote kilichosajiliwa na kinachombulika na Serikali.
  • Pia awe amepata angalau ufaulu wa “D” 4 za Kidato cha Nne(CSEE). Masomo ya Dini hayahusiki.
Ngazi ya Diploma ya Juu (NTA Level 6)
Sifa za Kujiunga:
  • Kidato cha Nne (Form Four) na ufaulu wa angalau daraja la nne (Division IV) na diploma ya NTA Level 5 katika kozi husika.
ANGALIZO:
  • Kozi ya Uhasibu na Fedha katika Serikali za Mitaa (Local Government Accounting and Finance) inahitaji mwombaji awe amefaulu somo la HISABATI katika mtihani wake wa kidato cha nne.
  • Kama mwombaji amefanya mtihani wa kidato cha nne zaidi ya mara moja, aambatanishe nakala za vyeti vyake vya awamu zote za mithani aliyofanya.
Gharama za masomo na mchanganuo wa ada unapatikana katika ukurasa wa
tatu(3) wa fomu ya maombi.
Fomu zinapatikana:
  • Chuoni, Hombolo
  • Kampasi ya Dodoma Mjini (Area C)
  • Katika tovuti ya Chuo www.lgti.ac.tz
  • Wizarani Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Library)
Fomu iliyokwisha jazwa iambatanishwe na malipo ya ada ya maombi ya shilingi
10,000/=kwenye Akaunti Na. 50501100209 NMB. Jina la akaunti ni CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA
Taarifa zaidi Tembelea Website ya Chuo cha Serikali za Mitaa http://www.lgti.ac.tz

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!