Sead Ramovic Kocha Mpya Yanga Sc
Sead Ramovic Kocha Mpya Yanga Sc
Klabu ya Yanga imemtambulisha Sead Ramovic raia wa Ujerumani kuwa kocha wao Mpya akirithi mikoba ya Miguel Angel Gamondi.
Kabla ya Young Africans Sead Ramovic alikuwa Kocha mkuu wa timu ya Ts galaxy ya Afrika ya kusini.
Sead Ramovic mwenye umri wa miaka 45 akiwa kama mchezaji alicheza kama golikipa kwenye vilabu kadhaa nchini kwao Ujerumani.

Sead Ramovic Kocha Mpya Yanga Sc
CV ya Sead Ramovic Kocha Mpya wa Yanga Sc 2024
Ramovic hana historia kubwa sana kwenye ukocha maana ameifundisha klabu moja tu ya Afrika Kusini TS Galaxy ambayo amekua nao toka mwaka 2021 mpaka mwaka huu 2024 .
Aidha TS Galaxy ambayo ametokea msimu huu wa 2024/2025 inashika nafasi mwisho kwenye Msimamo wa Ligi (South African Premiership)
Katika Mechi sita alizoiongoza Klabu hiyo haijashinda mchezo hata mmoja, ikipoteza minne na kutoa sare mbili, huku ikiwa na pointi mbili tu.
Sead Ramovic ni muumini wa mfumo wa 4-2-3-1.

Sead Ramovic Kocha Mpya Yanga Sc
