RATIBA ya Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mzunguko wa Sita

Filed in Habari by on 01/10/2024 0 Comments
RATIBA ya Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mzunguko Wa sita

RATIBA ya Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mzunguko wa Sita

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kuwa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Zanzibar utafanyika kuanzia tarehe 07 hadi 13 Oktoba, 2024.
Akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi Kisiwani Pemba, Zanzibar, Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk amesema kuwa uboreshaji huo utajumuisha mikoa ya Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja , Kusini Unguja , Kaskazini Pemba na Kusini Pemba .
Jaji Mbarouk amesema kuwa uboreshaji huo ambao unafanyika kwenye mzunguko wa sita kwa mujibu wa kalenda ya Tume kwa upande wa Zanzibar utahusu kuwaandikisha watanzania wote wanaoishi Zanzibar ambao wanastahili kuandikishwa kuwa wapiga kura kwaajili ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Naye Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu Asina Omari, amesema kuwa kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na.1 ya Mwaka 2024, Tume itawaandikisha watanzania waliopo Zanzibar ambao wametimiza umri wa miaka 18 na zaidi au watakaotimiza umri huo wakati au kabla ya tarehe ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Ameongeza kuwa mtanzania huyo atakeyandikishwa ni lazima awe hajapoteza sifa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi au sheria nyingine yeyote na awe anastahili kuandikishwa kuwa mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
“Kwa lugha nyepesi ni kwamba, Tume itamwandikisha mtanzania yeyote aliyopo Zanzibar ambaye amekosa sifa za kuandikishwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC). Hivyo, atakayeandikishwa kwenye Daftari la Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi atapiga kura moja tu ya kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Jaji Asina.
Uzinduzi wa uboreshaji wa Daftari ulifanyika tarehe 20 Julai, 2024 mkoani Kigoma na mpaka sasa uboreshaji umeshafanyika kwenye mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Manyara, Singida na baadhi ya Wilaya za mkoa wa Dodoma.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!