RASMI Yanga yaachana na Miguel Gamondi
RASMI Yanga yaachana na Miguel Gamondi
Uongozi wa Young Africans Sports Club umefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza, Angel Miguel Gamondi.
Vilevile, Uongozi wa Young Africans Sports Club, umesitisha mkataba wa kocha msaidizi wa kikosi cha kwanza, Moussa Ndaw.
Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuwashukuru Makocha hao kwa mchango wao ndani ya Klabu hiyo na unawatakia kila la kheri katika majukumu yao mapya.
Tayari mchakato wa haraka wa kutafuta Makocha wapya wa kikosi chetu cha kwanza umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde.

RASMI Yanga yaachana na Miguel Gamondi
