RAIS Samia Alipia tiketi zote Stars vs Guinea Kufuzu AFCON 2025

Filed in Michezo by on 19/11/2024 0 Comments

RAIS Samia Alipia tiketi zote Stars vs Guinea Kufuzu AFCON 2025RAIS Samia Alipia tiketi zote Stars vs Guinea Kufuzu AFCON 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa ruhusa kwa Watanzania kuingia uwanjani bure leo Novemba 19, 2024 ili kuunga mkono timu ya Taifa (Taifa Stars) itakapokuwa ikikabili Guinea.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mchezo huo ni wa mwisho utakaoamua nafasi ya Tanzania kushiriki AFCON 2025 itakayofanyika nchini Morocco.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, wakati akizungumza katika maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa na miaka 60 ya kifo cha Sheikh Kaluta Amri Abedi, yaliyofanyika Novemba 18, 2024, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Mwinjuma amesisitiza umuhimu wa mchezo huo katika kufuzu kwa mashindano ya AFCON 2025, akisema, “Tuna maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu uzito wa mchezo huu. Mchezo huu ndio unaamua kama tunafuzu kwenda kucheza AFCON 2025 kabla ya kuandaa ya kwetu mwaka 2027.”

Aidha, alitoa wito kwa Watanzania kwenda uwanjani kwa wingi ili kuunga mkono timu yao kwa kuwa hakutakuwa na kiingilio, akiongeza, “Mhe. Rais ametuelekeza tuwaruhusu na kuwahimiza ndugu zetu Watanzania kwenda kuiunga mkono na kuishangilia timu yao, na hakuna mtu atakayelipa chochote kwa hisani ya Mhe. Rais.”


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!