RAIS Samia Afanya Uteuzi Mpya Leo 11 November 2024

Filed in Habari by on 11/11/2024 0 Comments

RAIS Samia Afanya Uteuzi Mpya Leo 11 November 2024RAIS Samia Afanya Uteuzi Mpya Leo 11 November 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

Prof. Harun Jeremia Mapesa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Kabla ya uteuzi huu, Prof. Mapesa alikuwa Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Mzumbe, anachukua nafasi ya Prof. Shadrack Mwakalila ambaye amemaliza muda wake.

Rais Samia pia amemteua Mhandisi Peter Rudolf Ulanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL). Mhandisi Ulanga anachukua nafasi ya Mhandisi Ladislaus Matindi ambaye amestaafu.

Uteuzi huu umeanza tarehe 09 Novemba, 2024.RAIS Samia Afanya Uteuzi Mpya Leo 11 November 2024


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!