RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MPYA

Filed in Habari by on 08/09/2024 0 Comments

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MPYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

Bw. Salim Ramadhani Msangi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA). Kabla ya uteuzi huu, Bw. Msangi alikuwa akikaimu nafasi hiyo; na

Bw. Abdul Athumani Mombokaleo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mombokaleo alikuwa Meneja wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), anachukua nafasi ya Bw. Mussa Mbura ambaye atapangiwa majukumu mengine.

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MPYA


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!