ORODHA ya Majukwaa na Applications Zilizofungiwa Kujihusisha na Utoaji wa Mikopo Kidijitali
ORODHA ya Majukwaa na Applications Zilizofungiwa Kujihusisha na Utoaji wa Mikopo Kidijitali
Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuufahamisha Umma kuwa imebaini kuwepo kwa Majukwaa na Programu Tumizi ‘Applications” zinazojihusisha na utoaji wa mikopo kidijitali bila ya kuwa na leseni na idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania.
Aidha, Majukwaa na Programu hizo zimeshindwa kukidhi matakwa ya Mwongozo kwa Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa Daraja la Pili wanaotoa huduma za mikopo kwa njia ya kidijitali wa mwaka 2024 uliotolewa na Benki Kuu tarehe 27 Agosti, 2024 (Guidance Note on Digital Lenders Under Tier 2 Microfinance Service Providers, 2024).
Mwongozo huo unalenga kuimarisha usimamizi wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha Daraja la Pili nchini na kuhakikisha uzingatiwaji wa Kanuni za Kumlinda Mlaji wa Huduma za Fedha, ikijumuisha uwazi, uwekaji wa tozo na riba, njia za ukusanyaji wa madeni, na utunzaji wa taarifa binafsi za wateja na kulinda faragha zao.
Kupitia taarifa hii, Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuarifu Umma kwamba Majukwaa na Programu Tumizi “Applications” zifuatazo hazina kibali na haziruhusiwi kuendelea na shughuli za utoaji mikopo kidijitali;

ORODHA ya Majukwaa na Applications Zilizofungiwa Kujihusisha na Utoaji wa Mikopo Kidijitali

ORODHA ya Majukwaa na Applications Zilizofungiwa Kujihusisha na Utoaji wa Mikopo Kidijitali
Benki Kuu inautahadharisha Umma kutojihusisha na Majukwaa na Progamu Tumizi “Applications” hizo.
Aidha, Benki Kuu inashirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzifungia programu hizi ili kuepusha Umma kutumia huduma za fedha zisizokuwa na vibali vya Mamlaka husika.
Benki Kuu imechapisha na itaendelea kuhuisha orodha ya watoa huduma walioidhinishwa kutoa huduma za mikopo katika tovuti yake.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na: Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Benki Kuu ya Tanzania, 2 Mtaa wa Mirambo, S.L.P 2939, 11884 Dar es Salaam, Simu Na. +255 22 223 5586; Barua Pepe: info@bot.go.tz
Emmanuel M. Tutuba
GAVANA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: ORODHA ya Majukwaa na Applications Zilizofungiwa Kujihusisha na Utoaji wa Mikopo Kidijitali