NAFASI za Walimu Evangelistic Pre-& Primary School
NAFASI za Walimu Evangelistic Pre-& Primary School
Uongozi wa shule ya Tumaini Evangelistic Pre-& Primary School – Moshi iliyopo Langasani unapenda kuutangazia umma kuwa, shule imetoa nafasi za ajira kwa walimu na Mhasibu.
SIFA ZAWAOMBAJI:
✅Walimu wa shule ya Msingi.
- Wenye stashahada au shahada ya ualimu kwa somo la kiingereza (English)
- Wenye uzoefu usiopungua miaka miwili (02) katika ufundishaji wa madarasa ya mitihani kwa shule za private (English Medium)
✅Walimu wa madarasa ya awali.
- Wenye astashahada au stashahada ya ualimu.
- Wenye uzoefu usiopungua miaka miwili (02) katika ufundishaji wa madarasa ya awali (Baby class, Middle class and Pre-unity class)
✅Mhasibu.
- Awe na astashahada au stashahada ya uhasibu.
- Awe na uzoefu usiopungua mwaka mmoja (01).
MASHARITI YA JUMLA YA NAFASI ZOTE ZA KAZI:
- Waombaji wote wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 35.
- Waombaji wote wawe ni wakristo waliookoka, kwani shule ni ya mlengo na malezi ya kidini.(Pentekoste)
- Waombaji waambatanishe nakala za vyeti vya taaluma, cheti cha kuzaliwa na barua ya utambulisho kutoka kwa Mchungaji wako.
N.B: Maombi yote yaandikwe kwa lugha ya kiingereza na yaletwe shuleni au yatumwe kupitia email ya shule, “tumainievangelistic@gmail.com“.
Waombaji wenye sifa tajwa ndio watakaoitwa kwa mahojiano zaidi.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 06/12/2024.
