NAFASI za Walimu EG White Secondary School
NAFASI za Walimu EG White Secondary School
Ofisi ya Meneja wa shule ya EG White Secondary School Dodoma, inapenda kuutangazia umma kuwa shule imetoa nafasi ya ajira kama ifuatavyo:-
Walimu
Waajiriwa katika nafasi hii wanatakiwa kuwa wenye sifa zifuatazo:-
Wenye stashahada au shahada ya elimu na uzoefu katika masomo yafuatayo
- Physics
- Mathematics
- Civics
- Chemistry
- Geography
- English
- Biology Literature
- ICS
- Kiswahili
- History
Wenye ujuzi wa ziada kama muziki, mazingira, michezo, TEHAMA, MG, SYL na ufundi.
Mpishi
Patron
- Umri usiopungua miaka 30 na usiozidi miaka 50.
- Mwenye Elimu ya malezi ya watoto atafikiriwa kwanza.
- Elimu ya kidato cha nne na kuendelea.
- Uwezo wakuongea na kuandika lugha ya Kingereza kwa ufasaha.
- Mwenye upendo kwa watoto na mvumilivu katika kazi ya malezi ya watoto.
- Anayemcha Mungu na mwenye maadili mema.
- Mwenye uwezo wa kufundisha michezo kama sifa ya ziada lakini siyo lazima.
- Mwenye uzoefu wa kushughulika na watoto wa rika zote (MG, SYL).
Masharti ya jumla.
- Waombaji wote waambatanishe maombi yao na vivuli vya cheti cha kuzaliwa na kitambulisho cha NIDA.
- Waombaji waambatanishe maelezo yao binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anwani, namba ya simu ya kuaminika, pamoja na majina matatu ya wadhamini wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vivuli vya vyeti vya taaluma pamoja na picha moja ya passport iliyopigwa hivi karibuni.
- Maombi yaandikwe kwa lugha ya kiingereza.
Zingatia
Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono na zitumwe kwenye barua pepe info@ews.sc.tz au anwani tajwa hapa chini.
SCHOOL MANAGER
EG WHITE SECNDARY SCHOOL
P.O BOX 3118
DODOMA
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 10/12/2024.
