NAFASI ZA KAZI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024 ITIGI DISTRICT COUNCIL

Filed in Ajira by on 16/09/2024 0 Comments
NAFASI ZA KAZI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024 ITIGI DISTRICT COUNCIL

NAFASI ZA KAZI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024 ITIGI DISTRICT COUNCIL

Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi anawatangazia Watumishi wa Umma wote nafasi za kazi kwa ajili ya shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024.
NAFASI ZINAZOTANGAZWA:-
  • Msimamizi wa Kituo
  • Afisa Mwandikishaji wa Wapiga kura
SIFA ZINAZOTAKIWA
  • Asiwe na dhamana au uongozi katika chama chochote cha siasa
  • Awe ni Mtumishi katika Utumishi wa Umma (Public Service). (c) Awe Mwadilifu.

NAMNA YA KUANDIKA BARUA

  • Barua zote ziandikwe kwa mkono
  • Barua iandikwe majina kamili yanayotumika katika Utumishi Barua itaje nafasi ya kazi unayoomba.
  • Barua itaje cheo katika Utumishi wa Umma
  • Barua itaje kituo cha kazi
  • Barua iwe na anuani kamili ikiwa na namba ya simu inayopatikana wakati wote 
  • Barua iambatishwe na maelezo binafsi (CV)
  • Barua ziwasilishwe kwa mkono masijala ya wazi ya Mkurugenzi Mtendaji Itigi.
Barua iandikwe kwa:
Msimamizi wa Uchaguzi,
Halmashauri ya Wilaya ya Itigi,
S.L.P 70, ITIGI.
Mwisho wa kupokea barua hizo ni tarehe 17 Septemba, 2024 siku ya Jumanne saa 9.30 Alasiri.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!