NAFASI Za Kazi Tunduma Town Council

NAFASI Za Kazi Tunduma Town Council
NAFASI Za Kazi Tunduma Town Council
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma anawatangazia wananchi wote wenye sifa zilizoainishwa kwenye tangazo hili kuomba nafasi za kazi ya mkataba wa miezi mitatu (03) ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri.
✅WAKUSANYA USHURU (MAKARANI) – NAFASI 90
KAZI NA MAKUMU.
- Kukusanya Mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kutumia Mashine za Kielectronic za kukusanyia Mapato (POS)
- Kuhakikisha Fedha inayokusanywa inapelekwa Bank katika akaunti za Halmashauri kwa wakati
- Kuhakikisha Mapato yote yanayopaswa kukusanywa na Halmashauri yanakusanywa kwa usahihi
- Kutunza kumbukumbu za Hesabu
- Kutunza vizuri mashine za kukusanyia Mapato (POS)
- Kutoa na kuwasilisha taarifa za makusanyo ya kila siku kwa Halmashauri
- Kufanya kazi nyingine atakazo pangiwa na Msimamizi wake
NB: MSHAHARA KWA MWEZI SHILINGI 200,000 (LAKI MBILI KWA MWEZI)
Kuajiriwa wenye Elimu ya kuanzia Astashahada (Certificate) na kuendelea ambao wana uelewa wa kutumia simu janja (Smart phone), sababu Mapato yote ya Serikali yarıakusanywa kwa kutumia Mashine za Kielectronic za Kukusanyia Mapato (POS) ambayo ina application sawa na simu janja.
Aidha waombaji wenye sifa zaidi ya zilizotajwa hapo juu maombi yao hayatafikiriwa
MASHARTI YA WAOMBAJI KATIKA KAZI HII
- Awe ni raia wa Tanzania
- Awe amehitimu kidato cha Nne /sita
- Asiwe Mwajiriwa wa Serikali
- Awe na Umri wa kati ya 18-45
- Muadilifu asiye na Kasoro yoyote
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina mawili ya Wadhamini Watumishi wa Umma (Referees) na anwani zao sahihi na namba za simu.
- Maombi yaambatane pamoja na nakala ya vyeti vyote vya kitaaluma, na Cheti cha kuzaliwa vya Mwombaji.
- Awe na Kitambulisho cha Taifa / Namba ya NIDA
- Awe tayari kupangiwa kituo chochote cha kukusanya Mapato ndani ya Mji wa Tunduma.
- Awe Muaminifu katika kukusanya Mapato ya Serikali na kuhakikisha fedha ya Serikali haipotei.
- Awe tayari kutii na kufuata maelekezo atakayopangiwa bila kuvunja misingi ya Sheria ndogongo za Halmashauri.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI:
Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono zikiwa na anwani kamili ya Mwombaji pamoja na namba ya simu na zitumwe kwa anuani ifuatayo;
MKURUGENZI WA MJI,
S.L.P 73,
TUNDUMA.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 17/01/2025 saa 9:30 Alasiri
