NAFASI za Kazi Musoma Municipal Council

Filed in Ajira by on 21/11/2024 0 Comments

NAFASI za Kazi Musoma Municipal CouncilNAFASI za Kazi Musoma Municipal Council

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma amepokea kibali cha ajira kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Hivyo anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa nafasi tatu (3) kama
zilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa:-

✅DEREVA DARAJA LA II NAFASI 03

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kupeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
  • Kufanya marekebisho madogo madogo ya gari.
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari
  • Kufanya usafi wa gari na
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

SIFA ZA MWOMABAJI
Awe na elimu ya kidato cha nne na Leseni daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usioupungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya uendeshaji magari (Basic driving Course) yanayotolewa na Chuo cha mafunzo ya ufundi stadi (VETA) au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Mshahara utalipwa kwa kuzingatia viwango vya Serikali TGS B

✅MHUDUMU WA JIKONI DARAJA LA II NAFASI (02)

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kusafisha vyombo vya kupikia
  • Kusafisha vyombo vya kulia chakula
  • Kusafisha sehemu ya kulia chakula
  • Kuwatayarishia Wapishi/Waandazi vifaa vya kazi
  • Kusafisha maeneo ya kupikia

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV wenye cheti cha mafunzo ya uhudumu wa jikoni cha mwaka mmoja (1) kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.

MSHAHARA: Mshahara utalipwa kwa kuzingatia viwango vya Serikali TGOS A

✅MSAIDIZI WA MAENDELEO YA JAMII DARAJA LA II– NAFASI 01

KAZI YA MAJUKUMU

  • Kuratibu shughuli za maendeleo katika Mtaa zikiwemo za wanawake na watoto na zikizingatia jinsia.
  • Kuwezesha jamii kushiriki katika kubuni kupanga, kutekeleza, kusimamia, kutathimini mipango/ miradi ya maendeleo.
  • Kuhamasisha na kuwawezesha wananchi kupanga, kutekeleza kazi za maendeleo ambazo ni pamoja na usafi wa mazingira, ujenzi wa shule, zahanati, majosho na ujenzi wa nyumba bora
  • Kuratibu shughuli za kupambana na UKIMWI
  • Kuratibu shughuli za Mashirika na Asasi zisizo za Kiserikali na za kijamii.
  • Kusaidia shughuli za kinga za magonjwa ya watoto wadogo eneo la kituo
    Kuwa kiongozi wa kituo cha kulea watoto

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliofuzu mafunzo ya cheti kwenye fani ya Maendeleo ya Jamii katika vyuo vya Maendeleo ya Jamii au vyuo vingine
vinavyotambuliwa na Serikali.

MSHAHARA: Mshahara utalipwa kwa kuzingatia viwango vya Serikali TGS B

MASHARTI YA JUMLA

  • Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 na usiopungua umri wa miaka 18
  • Waombaji wote waambatanishe na cheti cha kuzaliwa
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi “CV” yenye anuani na namba za simu na majina ya wadhamini (Referees) wa kuaminika
  • Waombaji wote waweke nakala za vyeti vya taaluma, na vyeti vya kidato cha Nne na sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika kwenye ajira portal.
  • Testimonials “Provisional result”, “Statement of Result”, hati za matokeo ya matokeo ya kidato cha Nne na Sita HAVITATAKUBALIWA
  • Waombaji wote waweke picha mbili “passport Size”, ya hivi karibuni katika ukurasa
    wa ajira portal
  • Waombaji wote waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na mamlaka husika ya TCU, NACTE na NECTA).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

MUHIMU Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;-
MKURUGENZI WA MANISPAA,
HALMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA,
S.L.P 194,
MUSOMA

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anwani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa.‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30/11/2024.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!