NAFASI za Kazi Mbulu District Council November 2024
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU 15-11-2024
Mkurugenzi amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2023/2024 chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kufuatia kibali hicho Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mbulu anakaribisha maombi kwa
watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi zifuatazo :-
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II NAFASI TATU (03)
MAJUKUMU YA KAZI
- Kuorodhesha barua zinazoingia masijala mwenye regista (Incoming
Correspondence Register) - Kuorodhesha barua zinazo toka nje yaTaasisi (Outgoing Correspondence Register)
- Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers)
- Kupokea majalada yanayo rudi masijala kutoka kwa watendaji
- Kutafuta kumbukumbu/Nyaraka au majalada yanayo hitajika na watendaji
- Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (Racks/Filling Cabinets) au Mahali pengine yanapo hifadhiwa.
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi(File tracking)
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Elimu ya kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya
stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya utunzaji wa kumbukumbu
kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kutumia kompyuta
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali– TGS C
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II NAFASI TATU (03)
MAJUKUMU YA KAZI
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri
- Kupokea Wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu
wanapoweza kushughulikiwa. - Kutunza taarifa za kumbukumbuka za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa
majukumu ya kazi - Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/
Kitengo/ sehemu husika - Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi
- Kufanya kazi nyingine atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
SIFA ZAMWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne (Form IV) au cha Sita (Form VI), wenye
stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha (NTA Level 6) ya uhazili. Aidha
wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kingereza maneno 100
kwa dakika moja na kupata program za kompyuta za ofisi kama vile; Word,
Excel, PowerPoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali -TGS C.
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini – Serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) yenye Anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya
barua pepe (E-mail adress) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
“Provisional “/Testimonials”/ “Statement of results” na hati za matokeo za kidato cha Nne na Sita (Form IV and Form VI results slip) HAVITAKUBALIWA. - Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma, wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
kuzingatia sifa za kazi husika. - Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Dilpoma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards)
- Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA au NACTVET).
- Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria. - Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.
MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu
S.L.P 74
MBULU
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa “Recruitment Portal”
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKILIWA
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 23 Novemba, 2024.
