NAFASI za Kazi Kutoka Corazon Sports Lounge
✅Meneja wa Bar (Bar Manager)
Majukumu ya Meneja wa Bar
- Kushughulika na matatizo ya wateja kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
- Kusimamia usafi wa vifaa vyote vya bar na mazingira kwa ujumla.
- Kufunga na kufungua hesabu ya mauzo kila siku.
- Kuagiza vinywaji.
- Kusimamia majukumu na wajibu kwa kila mfanyakazi ili kufikia malengo.
- Kusimamia utayarishaji na uwasilishaji wa vinywaji ili kufikia viwango vilivyowekwa
- Kushughulika na uboreshaji wa bidhaa na huduma.
- Kuratibu na kudumisha mawasiliano ya mara kwa mara baina ya wafanyakazi na uongozi
- Kupanga na kutekeleza mipango itakayoongeza mauzo na mapato.
✅Wahudumu(waiters/waitresses)
Majukumu ya wahudumu
- Kuandaa meza na kuweka sahani, glass sawa.
- Kusalimia wateja na kuwasindikiza katika meza wanazoenda kukaa.
- Kuwapa wateja Menu ya chakula na vinywaji pamoja na maelezo yaliyopo kwenye menu.
- Kupokea orders za wateja.
- Kuhudumia wateja chakula na vinywaji.
- Kusafisha meza na kupanga vitu upya pale pindi mteja anapoondoka.
- Kuwasilisha bili kwa wateja na kushughulikia malipo ya pesa kwa cash ama kwa kadi
✅Mtu wa Kufanya Usafi (Cleaner)
Majukumu ya Cleaner
- Kusafisha na kupangilia
- Kudumisha usafi wa vifaa na kuhakikisha vinafanya vizuri na vinaendelea kuwa safi.
- Kuthibiti taka zote zilizopo, pamoja na ukusanyaji na utupaji wa taka kwa bjia inayofaa ili kuepuka uchafuzi wa mazingira na kuzuia magonjwa
- Kuhakikisha viwango na sera zote za afya, usalama na usafi kwenye eneo vinazingatiwa.
- Kuhakikisha kuwa vifaa vya usafi kama vile sabuni na karatasi za chooni vipo kwa wingi
✅Mhasibu (Accountant)
Majukumu ya Mhasibu
- Kukusanya,kuchambua na kutoa taarifa za fedha mara kwa mara,kama vile taarifa za faida na hasra ,kufunga mahesabu.
- Kufuata sheria na kanuni zote za kuendesha biashara,ikiwa ni pamoja na kuhakikisha lesseni na vibali vyote vinalipiwa kwa wakati kulingana na miongozo ya serikali.
- Kusimamia matumizi ya ofisi, kuhakikisha vifaa vya ofisi vinanuliwa, kuhakikisha malipo na ada mbalimbali zinalipwa kwa wakati.
- Kuwasilisha takwimu kwa Mkurugenzi na kutunza kumbukumbu saihi za kifedha.
- Kusimamia miamala na mahesabu na kutoa taarifa ya kila siku.
NAFASI za Kazi Kutoka Corazon Sports Lounge
Jinsi ya kufanya Maombi
Maombi yote yatumwe kupitia mawasiliano yafuatayo WhatsApps number: +255 745 511 511 au email hii:
corazonagroup@yahoo.com

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Post Views: 85