NAFASI ZA KAZI KUSIMAMIA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024 DODOMA CITY TOWN
NAFASI ZA KAZI KUSIMAMIA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024 DODOMA CITY TOWN
Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma anawatangazia Watumishi wa Umma wote nafasi za kazi kwa ajili ya shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024.
NAFASI ZINAZOTANGAZWA NI: –
- Msimamizi wa Kituo
- Afisa Mwandikishaji wa Wapiga kura
SIFA ZINAZOTAKIWA
- Asiwe na dhamana au uongozi katika Chama chochote cha Siasa
- Awe ni Mtumishi katika Utumishi wa Umma (Public Service)
- Awe Mwadilifu
- Namna ya kuandika barua
- Barua zote ziandikwe kwa mkono
- Barua iandikwe kwa majina kamili yanayotumika katika Utumishi wa Umma
- Barua iainishe nafasi ya kazi unayoomba
- Barua iainishe cheo chako katika Utumishi wa Umma
- Barua iainishe kituo cha kazi
- Barua iandikwe anuani kamili ikiwa na namba yasimu inayopatikana wakati wote
- Barua iambatishwe na taarifa binafsi (CV)
- Barua ziwasilishwe kwa mkono Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma
Barua iandikwe kwa anwani ifuatavyo: –
Msimamizi wa Uchaguzi,
Halmashauri ya Jiji la Dodoma,
S.L.P. 1249,
DODOMA.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 23 Septemba, 2024 saa
9:30 alasiri.
