NAFASI Za Kazi Kakonko District Council

NAFASI Za Kazi Kakonko District Council
NAFASI Za Kazi Kakonko District Council
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko anayo furaha kutangaza nafasi 26 za ajira ya Mkataba kwa wananchi wa Kakonko wote wenye sifa stahiki nafasi ya Wakusanya Mapato
SIFA ZA KUAJIRIWA.
- Awe amehitimu kidato cha nne (4)
- Awe na umri kuanzia miaka kumi na nane (18) hadi Arobaini na tano (45)
- Awe na Kitambulisho cha Nida au Namba ya Nida
- Awe anaweza kutumia simu janja
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
- Waombaji wote wawe na umri kati ya miaka 18 – 45.
- Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti cha kuazaliwa.
- Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi (CV) yenye anuani na namba za simu za kuaminika na majina mawili ya wadhamini.
- Maombi yaambatishwe na picha moja (Passport size ya hivi karibuni na iandikwe jina kwa nyuma).
- Waombaji wote waambatishe nakala ya kitambulisho cha Taifa (NIDA) kwa ambao hawana vitambulisho hivyo, namba za NIDA ziandikwe kwenye maelezo (CV).
Waombaji wote waambatishe nakala ya cheti cha kidato cha nne (4) Maombi yote yawasilishwe Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwa anuani ifuatayo:-
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 03,
KAKONKO.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 21/01/2025 saa tisa alasiri.
