NAFASI za Kazi Jeshi la Uhamiaji Tanzania
NAFASI za Kazi Jeshi la Uhamiaji Tanzania
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwa Mamlaka aliyonayo chini ya Kanuni Namba 11(1) ya Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018, ametangaza nafasi za Ajira Mpya za Askari wa Uhamiaji kwa Vijana wa Kitanzania wenye sifa zifuatazo:-
Sifa Za Mwombaji
- Awe ni raia wa Tanzania;
- Awe hana ajira au hajawahi kuajiriwa na Taasisi yoyote Serikalini;
- Awe na Cheti cha Kuzaliwa;
- Awe na Kitambulisho cha Taifa au Namba ya Utambulisho iliyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA);
- Awe na siha njema ya mwili na akili.
- Awe hajawahi kutumia Dawa za kulevya;
- Asiwe na kumbukumbu au Taarifa zozote za kuhusika katika masuala au matukio ya uhalifu au jinai;
Asiwe na alama yoyote au michoro (Tatoo) katika mwili wake; - Awe hajaoa au kuolewa wala kuwa na mtoto;
- Mwombaji mwenye Elimu ya Kidato cha Nne awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 22, Mwombaji mwenye Elimu ya Kidato cha Sita na Stashahada awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 25 na Mwombaji mwenye Elimu ya Shahada/ Stashahada ya Juu awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 30.
- Awe tayari kufanya kazi za Idara ya Uhamiaji mahali popote Tanzania.
- Awe tayari kujigharimia katika hatua zote za ufuatiliaji na uendeshwaji wa zoezi la Ajira.
Maombi yatakayopewa Kipaumbele:
Maombi yatakayopewa kipaumbele ni ya waombaji wenye taaluma ngazi ya Shahada/Stashahada ya Juu, Stashahada na Astashahada kutoka katika Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali wenye fani zifuatazo:-
Mtaalamu wa Lugha za Kimataifa, Utawala, Sheria, Uhusiano, TEHAMA, Masijala, Ukatibu Mahsusi, Uhasibu, Ununuzi na Ugavi waliosajiliwa na Bodi, Takwimu, Uchumi, Umeme, Ufundi wa Magari, Ufundi wa AC, Cyber Security, Brass band, na Mpiga chapa (Printer).
Jinsi ya Kutuma Maombi:
Maombi yote ya Ajira yatawasilishwa kupitia tovuti ya Idara ya Uhamiaji ambayo ni https://www.immigration.go.tz kuanzia tarehe 29 Novemba, 2024 na mwisho wa kufanya maombi ni tarehe 13 Disemba, 2024.
Wakati wa kufanya Maombi, Mwombaji anatakiwa kuambatisha (upload) kwenye mfumo wa Ajira nyaraka zifuatazo zilizo katika mfumo wa PDF (kila Nyaraka moja isizidi 300Kb);
- Picha (passport size) ya hivi karibuni iliyo katika mfumo wa jpg/png isiyozidi 300Kb kwa ajili ya kuambatisha kwenye mfumo (upload);
- Barua ya maombi ya ajira iliyoandikwa kwa mkono;
- Barua ya Utambulisho toka Serikali ya Mtaa/Kijiji au Shehia; kwa walio Makambini JKT/JKU wawe na barua za Utambulisho kutoka kwa Mkuu wa Kambi;
- Cheti cha Kuzaliwa;
- Awe na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya NIDA kwa ajili ya kujisajili kwenye mfumo;
- Awe na Index namba za vyeti vya kufaulu Kidato cha Nne na Kidato cha Sita ambazo atajaza kwenye mfumo wa ajira;
- Vyeti vingine vya kuhitimu fani mbalimbali ngazi ya Astashahada, Stashahada, na Shahada/Stashahada ya Juu (kama anavyo na viwe vimehakikiwa katika vyuo husika);
- Vyeti vya usajili wa taaluma kwa fani zinazohitaji usajili wa Bodi; ix.
- Wasifu wa Mwombaji (CV).
Tahadhari
Maombi yote yatapokelewa katika utaratibu ulioainishwa katika kifungu Namba 3 hapo juu na si vinginevyo;
Mwombaji yoyote atakayebainika kuwasilisha nyaraka za kughushi atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa Mahakamani;
Epuka Matapeli wanaoomba fedha au rushwa ya aina yoyote kwa ajili ya kusaidia kupata nafasi za Ajira.
