NAFASI za Kazi Iringa Municipal Council

Filed in Ajira by on 19/11/2024 0 Comments

NAFASI za Kazi Iringa Municipal CouncilNAFASI za Kazi Iringa Municipal Council

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuomba nafasi ya kazi iliyotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb Na. FA. 170/363/01A/116 cha tarehe 25 Septemba, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

✅MHUDUMU WA JIKONI DARAJA II- (NAFASI 4)

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kusafisha vyombo vya kupikia;
  • Kusafisha vyombo vya kulia chakula;
  • Kusafisha sehemu ya kulia chakula;
  • Kuwatayarishia Wapishi/Waandazi vifaa vya kazi;
  • Kusafisha maeneo ya kupikia.

SIFA ZA KUAJIRIWA
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) Mwenye cheti cha mafunzo ya mwaka mmoja ya Uhudumu wa Jikoni kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali

NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya mshahara ni TGOS A

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa
    kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/.Wakili;
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika
    kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
    watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na cheti cha taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne na
    cheti cha kuhitimu mafunzo ya Uhudumu wa jikoni.
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne (FORM IV AND RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Muhimu: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Mkurugenzi wa Halmashauri,
Manispaa ya Iringa,
S.L.P. 162,
IRINGA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 02/12/2024


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!