NAFASI za Kazi Ikungi District Council November 2024
NAFASI za Kazi Ikungi District Council November 2024
Kufuatia Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kupata kibali cha ajira mpya chenye Kumb. Na. FA. 170/366/01B/150 cha tarehe 26 Septemba, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Ikungi anatangaza nafasi ya kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye Sifa za kujaza nafasi kama ilivyoorodheshwa kwenye Tangazo hili.
✅MLEZI WA WATOTO MSAIDIZI – (NAFASI 1)
SlFA ZA MWOMBAJI:
Awe na Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI). Awe amefuzu mafunzo ya Astashahada/Cheti (Technician Certificate NTA level 5) katika moja ya fani zifuatazo: Elimu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto, Ustawi wa Jamii, Saikolojia kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III
- Kushiriki kutekeleza mpango jumui wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya watoto, (ECD integrated plan);
- Kuandaa na kutekeleza ratiba ya shughuli za kila siku katika kituo husika;
- Kubainisha na kutumia mazingira salama ya kujifunzia watoto;
- Kutoa rufaa ya masuala ya watoto yaliyo nje ya uwezo wake;
- Kutambua watoto wenye mahitaji maalumu na kutoa huduma stahiki;
- Kushiriki katika uhamasishaji wa jamii katika kutoa huduma za malezi, makuzi na maendeleo
ya awali ya mtoto; - Kutoa ushauri kwa wazazi/walezi kuhusu malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto
katika eneo lake; - Kuandaa na kutoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kila siku katika eneo husika;
- Kushiriki kwenye mchakato wa uendeshaji wa mashauri ya watoto katika ngazi husika (case management);
- Kuandaa taarifa ya uanzishaji wa vituo vya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto katika maeneo husika; na
- Kufanya kazi nyingine yoyote atakayopangiwa na Mkuu wake wa kazi kulingana na elimu na ujuzi wake.
NGAZI YA MSHAHARA: Mshahara wa kuanzia ni kima cha serikali katika ngazi ya TGS. B1
MASHARTI YA JUMLA:
- Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania na mwenye umri usiopungua Miaka Kumi na Nane
(18) na usiozidi miaka Arobaini na Tano (45). - Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha
kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti
ya Ajira katika Utumishi wa Umma - Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili
- Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya Wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma,maelezo,nakala za vyeti vilivyothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili ambavyo ni kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofika kiwango
hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. - Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificate, – vyeti vya kitaaluma (professional Certificate from respective boards)
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU/NACTE na NECTA)
- “Testimonials”, Provisional Results, Statement of Results, Hati za matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa
umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na.CAC45//257/01/D/140 wa tarehe.30 Novemba, 2010 - Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba isipokua kama
wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi - Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria
MUHIMU kumbuka kuambatanisha Barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya Elimu, Anuani ya Barua hiyo ielekezwe kwa;
MKURUGENZI MTENDAJI (W),
HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI,
S.L.P 42,
SINGIDA.
Maombi yote yatumwe kwenye Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia Anuani ifuatayo http://portal.ajira.go.tz, Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya
Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioidhinishwa katika Tangazo hili Hayatafanyiwa Kazi.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 28 Novemba 2024.
