NAFASI Za Kazi Christian Council of Tanzania (CCT)

NAFASI Za Kazi Christian Council of Tanzania (CCT)
NAFASI Za Kazi Christian Council of Tanzania (CCT)
Uongozi wa Chaplaincy ya Chuo Kikuu Cha Dodoma kupitia vikao vyake vitatu vya kanuni, yaani kamati Kuu, Kamati Tendaji na Baraza la Chaplaincy waliridhia kuwepo kwa nafasi moja (1) ya Mhasibu wa kujitolea (Treasurer volunteer).
Hivyo basi tunaomba wote waliohitimu ngazi ya shahada kuomba nafasi hii ya kujitolea ili kuujenga mwili wa Kristo katika Chaplaincy yetu.
WAJIBU WA MHASIBU
- Kupokea na kuingiza takwimu katika mfumo wa kiuhasibu kwa kufuata taratibu za Chaplaincy ya Chuo Kikuu Cha Dodoma
- Kupitia na kukagua taarifa za fedha kutoka kwa wahasibu wa vitivo
- Kufanya mlinganisho wa bank (Bank reconciliation)
- Kutoa maelezo yanayotakiwa kwa mujibu wa hoja za wakaguzi wa ndani
- Kuandaa taarifa za fedha
SIFA ZA MWOMBAJI WA NAFASI YA KAZI
- Awe raia wa Tanzania
- Awe ni Mkristo anayetokana na wana USCF
- Awe mwaminifu na mwadilifu
- Awe tayari kujitolea kwa malipo ya posho atakayokubaliana kati yake na Uongozi wa Chaplaincy
- Awe na moyo wa utayari katika kazi
- Awe aliyehitimu ngazi ya Shahada
- Awe na Shahada ya kwanza ya uhasibu / Accounting kutoka kwenye Chuo kinachotambulika na serikali
- Awe na uzoefu katika uandaji wa akaunti na ujuzi wa hesabu (Account preparation & Balance sheet).
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
Waombaji wenye sifa watume Barua za maombi ya kazi, Wasifu (CV) na Vivuli vya Vyeti Kupitia Barua Pepe:
BARUA PEPE: cetusefudomchaplaincy@gmail.com
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 28 Januari, 2025.
