NAFASI za Kazi Chama Cha Ushirika JAM MAONO LIMITED
NAFASI za Kazi Chama Cha Ushirika JAM MAONO LIMITED
Chama cha ushirika wa Akiba na Mikopo cha JAM MAONO LIMITED, Arusha katika mpango mkakati wake wa kupanua wigo wa kutoa huduma imeanzisha huduma za uwakala wa fedha kwa mitandao ya simu na huduma za uwakala wa benki kupitia ofisi zake zilizopo eneo la Kimandolu – Jimbo la Arusha Mashariki ya KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Kati.
Kufuatia kuanzishwa kwa huduma hii Chama kinatangaza nafasi ya kazi ya KARANI WA FEDHA “Cash Teller” atakayehusika na kutoa huduma hizi kwa Wanachama na Jamii inayotuzunguka.
SIFA ZA MUOMBAJI;
- Awe na uzoefu wa kazi husika kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.
- Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
Awe ni mhitimu wa elimu ya sekondari. - Awe Mkristo Mlutheri.
- Elimu ya Fedha kwa ngazi ya awali (Basic Technician Certificate in Finance) itakuwa sifa ya ziada.
- Umri kuanzia ya miaka 20 – 30.
- Awe na Wadhamini wawili wenye mali zisizohamishika.
- Barua za maombi ziambatanishwe na vivuli vya vyeti vya taaluma, wasifu wa muombaji “CV” pamoja na picha moja ndogo ya sasa ya muombaji.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 23/12/2024 na maombi yatumwe kwa njia ya posta au kuwasilishwa kwa mkono katika ofisi za chama Jimboni Kimandolu.
Maombi yatumwe kwa;
MWENYEKITI WA BODI
JAM MAONO SACCOS LIMITED
S.L.P 16838 – ARUSHA ARUSHA, TANZANIA
