NAFASI za Kazi Biharamulo District Council

Filed in Ajira by on 21/11/2024 0 Comments

NAFASI za Kazi Biharamulo District CouncilNAFASI za Kazi Biharamulo District Council

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo amepokea kibali cha Ajira ya Mkataba kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb Na FA.170/368/01 “C”/107 cha tarehe 17 Septemba, 2024.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Kwa hiyo, anawatangazia Watanzania wote wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 02 kama inavyoonekana hapa chini:-

✅DEREVA DARAJA LA II – (NAFASI 02) TGS B.

SIFA ZA MWOMBAJI:-
Kuajiriwa mwenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na leseni ya Daraja la E au C1 ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.

Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali. Waombaji wenye Cheti cha majaribio ya Ufundi Daraja la II watafikiriwa kwanza.

MAJUKUMU YA KAZI:-

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
  • Kufanya usafi wa gari.
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.

MASHARTI YA JUMLA KWA MWOMBAJI.

  • Mwombaji awe ni raia wa Tanzania na mwenye umri usiozidi miaka 45.
  • Mwombaji aambatanishe nakala ya Cheti cha kuzaliwa.
  • Mwombaji aambatanishe Nakala ya Kitambulisho cha Uraia au Namba ya Kitambulisho hicho kutoka mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo binafsi(CV), nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofika kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa.
  • Picha moja Passport size iandikwe jina kwa nyuma.
  • Hati za matokeo ya kidato cha nne na sita (Statement of Results havitakubalika).
  • Waombaji kazi ambayo tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe kazi hii.
  • Kazi hii ni ya Mkataba wa Mwaka mmoja tu.

Maombi yanaweza kuandikwa kwa lugha ya kiingereza au Kiswahili na yatumwe kwa njia ya posta kabla ya tarehe 02/12/2024 kwa anuani ifuatayo:-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 70, BIHARAMULO.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!