NAFASI 9 za Walimu Somo la Jokofu na Kiyoyozi

Filed in Ajira by on 14/12/2024

 

NAFASI 9 za Walimu Somo la Jokofu na KiyoyoziNAFASI 9 za Walimu Somo la Jokofu na Kiyoyozi

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

MWALIMU DARAJA LA III B – (REFRIGERATION AND AIR CONDITIONING) NAFASI 9

MKOA – KIGOMA 1, MANYARA 1, MARA 1, MOROGORO 1, MTWARA 1, RUKWA 1, RUVUMA 1, SHINYANGA 1, SIMIYU 1.

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na
    Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
  • Kutengeneza na Kufaragua zana za kufundishia na kujifunzia;
  • Kufundisha, kufanya Tathimini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi;
  • Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
  • Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi;
  • Kutoa ushauri wa kitaalamu na kitaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
  • Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za shule; na
  • Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye cheti cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita ambaye amefaulu masomo mawili au zaidi yanayofundishwa shuleni na kufaulu mafunzo ya Stashahada ya Ualimu ya miaka miwili (2) yenye somo la kufundishia la upoaji na viyeo vya hewa (Refrigeration and air conditioning) kutoka Vyuo vya Ualimu vinavyotambulika na Serikali.

AU Wenye Stashahada isiyo ya Ualimu katika fani ‘’Refrigeration and Air
Conditioning au Mechanical Engineering’’.

Waombaji ambao hawana somo la UALIMU ni lazima wawe tayari kupata mafunzo ya UALIMU baada ya kuajiriwa.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGTS- C

MASHARTI YA JUMLA.

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa
  • kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombiya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina yawadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato
    cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
    Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
    – Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
    – Computer Certificate
    – Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo zakidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa nakuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
    Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 20 Desemba, 2024


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Comments are closed.

error: Content is protected !!