NAFASI 84 za Kazi Shirika la Afya ICAP

Filed in Ajira by on 19/11/2024 0 Comments

NAFASI 84 za Kazi Shirika la Afya ICAPNAFASI 84 za Kazi Shirika la Afya ICAP Mkoa wa Geita

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita kwa kushirikiana na Shirika la ICAP imekuwa ikitekeleza Afua za kupambana na VVU/UKIMWI na Kifua kikuu katika Halmashauri zote za Mkoa wa Geita.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Inakaribisha maombi ya kazi ya Muda (Miezi kumi) kutoka kwa watanzania wenye Sifa, uwezo na Ujuzi wa taaluma za Afya.

Watumishi watapangiwa kufanya kazi katika Vituo vya Kutolea Huduma za Afya vilivyopo katika Halmashauri za Geita na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Nafasi zinazotangazwa ni kama ifautavyo:

✅WAUGUZI (ART NURSES) – NAFASI 28

MAJUKUMU.

  • Kutoa ushauri na elimu ya afya kwa wateja kuhusiana na upimaji wa maambukizi ya VVU, ufuasi sahihi wa huduma endelevu za dawa za kufubaza maambukizi pamoja na huduma jumuishi za tiba na matunzo katika kituo na jamii inayohudumiwa na kituo husika.
  • Kutoa ushauri na elimu ya afya kwa wanafamilia na walezi kuhusiana na mbinu za kudhibiti maambukizi mapya ya VVU.
  • Kuhakikisha wateja wanaohudhuria huduma za matunzo wanapata huduma bora kulingana na machaguo na matarajio yao kwa kuzingatia kanuni na taratibu za wizara ya afya.
  • Kuweka taarifa na kumbukumbu kwa ukamilifu na usahihi kwa huduma zote zilizotolewa kwa wateja.
  • Kutoa taarifa za utendaji na utekelezaji wa huduma jumuishi za 95-95-95 kulingana na viashiria vya huduma za kudhibiti maambukizi.
  • Kufanya majukumu mengine yote atakayoelekezwa na msimamizi wa kituo kulingana na ujuzi na maarifa ya mtumishi.
  • Kutoa tarehe za mahudhurio ya Kliniki za wateja Kushiriki katika uchukuaji wa sampuli za HVL.
  • Kuongoza ufuatiliaji na kuhakikisha ufuasi mzuri wa matibabu kwa kuwasimamia watoa Huduma ngazi ya jamii, ECs n.k

SIFA ZA MWOMBAJI.

  • Awe na Elimu na Cheti cha Kidato cha nne (IV) na waliohitimu mafunzo ya Astashahada/ Stashahada/ shahada katika Fani ya Uuguzi
  • Awe na uzoefu wa walau mwaka mmoja katika Kutoa huduma za Tiba na Matunzo katika vituo vya kutolea Huduma vilivyopo Mkoa wa Geita.
  • Awe na leseni hai ya kutoa Huduma (valid practice license).
  • Awe na uwezo wa kutumia kompyuta hasa program za MS word, excel, Powerpoint.
  • Ujuzi wa uchambuzi na utatuzi wa changamoto.
  • Uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha katika Kiingereza na Kiswahili.
  • Uwezo wa kufanya kazi kibinafsi na kama sehemu ya timu yenye usimamizi mdogo.
  • Uwezo wa kudumisha usiri katika nyanja zote.

WAPIMAJI VVU (HIV TESTERS) – NAFASI 37

MAJUKUMU.

  • Uhamasishaji na elimu juu ya uwepo wa Huduma za Kupima VVU (HTS) yaani kuelimisha wateja juu ya masuala yote ya magonjwa ya VVU na usimamizi wa matibabu pamoja na maisha ya kimsingi ya afya.
  • Kutumika kama kiunganishi kati ya matabibu/zahanati, watu waliopimwa na vituo vya matunzo.
  • Kutoa ushauri nasaha na kupima huku kukiwa na usiri na haki za mgonjwa, kutoa usaidizi wa kisaikolojia na kusaidia katika rufaa na uhusiano.
  • Kutathmini na kuandika marejeo yote, kufanya ufuatiliaji na kutoa taarifa juu ya matokeo ya rufaa.
  • Kufuatilia ubora (QA/QC) wa vifaa vya majaribio kwa nyenzo/sampuli za udhibiti kutoka idara ya maabara.
  • Kuhakikisha uhifadhi salama wa vitu vinavyohusiana na Upimaji VVU na kuomba/kutayarisha vifaa vyote vya matumizi vinavyohitajika kwa huduma za Upimaji VVU.
  • Kukusanya na kuwasilisha ripoti za Upimaji VVU kila siku, wiki, kila mwezi na robo mwaka kwa waratibu wa Upimaji VVU.
  • Kuweka Taarifa sahihi za upimaji VVU na kumbukumbu za rufaa/uhusiano (vitabu vya kumbukumbu, rejesta, ripoti).
  • Fanya kazi na mshiriki wa timu ili kufuatilia mipango ya uboreshaji wa ubora kuhusiana na malengo/ viashiria vya utendaji vilivyowekwa
  • Kuhakikisha upimaji wa VVU katika maeneo ya upimaji na kwenye jamii unafanywa kulingana na kanuni ya Kitaifa ya kupima VVU
    Kushiriki kikamilifu katika mpango wa Kitaifa wa EQA wa upimaji wa haraka wa
    VVU
  • Kuandika anuani sahihi za makazi mwa wateja wapya
  • Kutekeleza majukumu mengine yoyote ambayo yanaweza kuhitajika na kiongozi wake kulingana na ujuzi na maarifa ya mtumishi.

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Awe mwenye Elimu na Cheti cha Kidato cha nne (IV) na waliohitimu mafunzo ya Astashahada/ stashahada/shahada katika Fani ya Uuguzi/utabibu/maabara Awe na leseni hai ya Kutoa Huduma (valid practice license), muombaji mwenye mafunzo na cheti cha upimaji VVU atapewa kipaumbele
  • Mwenye uzoefu wa kufanya kazi walau mwaka mmoja katika vituo vya Tiba na Matunzo vilivyopo Mkoani Geita.
  • Ujuzi wa uchambuzi na utatuzi wa changamoto.
  • Uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha katika Kiingereza na Kiswahili.
  • Uwezo wa kufanya kazi kibinafsi na kama sehemu ya timu yenye usimamizi mdogo..Uwezo wa kudumisha usiri katika nyanja zote

✅AFISA MAABARA (LABORATORY SCIENTIST) – NAFASI 02

MAJUKUMU

  • Kutoa sampuli za vipimo vya maabara (HIV viral load ni kipaumbele),
  • Kutuma taarifa za wiki kwa mratibu wa huduma za maabara za TB, HVL na DBS. Kufanya uchunguzi wa vipimo vya maabara.
  • Kutunza kumbukumbu za majibu ya vipimo vya maabara.
  • Kuandaa na kutumia miongozo ya kufanyia vipimo vya upimaji.
  • Kusimamia utunzaji wa Kumbukumbu za matokeo ya vipimo vya maabara katika Rejesta.
  • Kutunza vifaa na Vitendea kazi vya Maabara.
  • Kusimamia na kufanya matengenezo kinga ya kila siku ya mashine za Maabara.
  • Kuthibitisha na Kutoa tafsiri ya matokeo ya vipimo vya maabara.
  • Kuhakiki na kuthibitisha njia mpya za uchunguzi wa kimaabara (new method validation and verification).
  • Kuhifadhi sampuli zinazotakiwa kufanyiwa uchunguzi au kupelekwa maabara za ngazi za juu.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Awe mwenye Elimu na Cheti cha Kidato cha nne (IV) waliohitimu mafunzo ya shahada katika Fani ya Maabara kutoka katika vyuo vinavyotambulika na Serikali.
  • Awe na Uzoefu wa kufanya kazi katika maabara zilizopo kwenye vituo vinavyotoa Huduma za Tiba na Matunzo vilivyopo Mkoa wa Geita kwa walau mwaka mmoja.
  • Muombaji aliyepata mafunzo ya Ubora wa maabara atapewa kipaumbele (laboratory quality management training)
  • Ujuzi wa uchambuzi na utatuzi wa changamoto.
  • Uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha katika Kiingereza na Kiswahili.
  • Uwezo wa kufanya kazi kibinafsi na kama sehemu ya timu yenye usimamizi mdogo.
  • Uwezo wa kudumisha usiri katika nyanja zote

✅MTEKNOLOJIA MAABARA NAFASI 06

MAJUKUMU

  • Kutoa sampuli ya vipimo vya maabara (HIV viral load ni kipaumbele).
  • Kutuma taarifa za wiki kwa mratibu wa huduma za maabara za TB, HVL na DBS.
  • Kufanya uchunguzi wa vipimo vya maabara.
  • Kutunza kumbukumbu za majibu ya vipimo vya maabara
  • Kuandaa na kutumia miongozo ya kufanyia vipimo vya upimaji.
    Kusimamia utunzaji wa
  • Kumbukumbu za matokeo ya vipimo vya maabara katika Rejesta.
  • Kutunza vifaa na Vitendea kazi vya Maabara.
  • Kusimamia na kufanya matengenezo kinga ya kila siku ya mashine za Maabara.
  • Kuthibitisha na Kutoa tafsiri ya matokeo ya vipimo vya maabara.
  • Kuhakiki na kuthibitisha njia mpya za uchunguzi wa kimaabara (new method validation and verification).
  • Kuhifadhi sampuli zinazotakiwa kufanyiwa uchunguzi au kupelekwa maabara za ngazi za juu.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI.

  • Awe mwenye Elimu na Cheti cha Kidato cha nne (IV) na aliyehitimu mafunzo ya Stashahada katika Fani ya Maabara kwa miaka mitatu (3) kutoka katika vyuo vinavyotambulika na Serikali.
  • Awe na Uzoefu wa kufanya kazi katika maabara zilizopo kwenye vituo vinavyotoa Huduma za Tiba na Matunzo kwa walau mwaka mmoja vilivyopo mkoani Geita.
  • Muombaji aliyepata mafunzo ya Ubora wa maabara atapewa kipauumbele (laboratory quality management training)
  • Ujuzi wa uchambuzi na utatuzi wa changamoto.
  • Uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha katika Kiingereza na Kiswahili.
  • Uwezo wa kufanya kazi kibinafsi na kama sehemu ya timu yenye usimamizi mdogo.
  • Uwezo wa kudumisha usiri katika nyanja zote

✅MFAMASIA (PHARMACIST) – NAFASI 01

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuainisha mahitaji ya mwaka ya dawa na vifaa na kuandaa bajeti yake.
  • Kuagiza,kununua, kuhifadhi na kusambaza dawa na vifaa tiba katika kituo chake cha kazi na kujua mifumo yote ya utumiaji na uagizaji wa dawa zikiwemo na dawa za wapokea huduma waishio na VVU.
  • Kuweka vizuri kumbukumbu za dawa za zana mbalimbali za mifumo ya dawa ikiwemo Pharmacy Module Database.
  • Kuandaa orodha ya dawa za hospitali (Hospital Fomulary) kwa matumizi ya kituo anapofanya kazi zikiwemo dawa za wapokea huduma waishio na VVU Kutoa dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa zikiwemo dawa za wapokea huduma waishio na VVU
  • Kusimamia matumizi sahihi ya dawa.
  • Kutengeneza dawa (compounding) kwa matumizi ya kituo anapofanya kazi. Kutoa taarifa juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya dawa (adverse drug reaction).
  • Kuelimisha watumishi walio chini yake, watumishi wengine wa sekta ya Afya na Jamii juu ya matumizi sahihi ya dawa.
  • Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Dawa zikiwemo dawa za wapokea huduma waishio na VVU katika kituo anapofanya kazi.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Awe mwenye Elimu na Cheti cha Kidato cha Nne (IV) na aliyehitimu mafunzo ya shahada katika Fani ya dawa (Pharmacy) kutoka katika vyuo vinavyotambulika na Serikali.
    Awe amesajiliwa na baraza la Famasi.
  • Awe na uzoefu wa kutumia wa Kompyuta hasa program za MS word, excel na powerpoint.
  • Mwenye uzoefu wa kufanya kazi katika vituo vya tiba na matunzo kwa walau mwaka mmoja vilivyopo Mkoani Geita.
  • Ujuzi wa uchambuzi na utatuzi wa changamoto.
    Uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha katika Kiingereza na Kiswahili.
  • Uwezo wa kufanya kazi kibinafsi na kama sehemu ya timu yenye usimamizi mdogo.
  • Uwezo wa kudumisha usiri katika nyanja zote

✅MTEKNOLOJIA DAWA (PHARMACEUTICAL TECHNICIAN) – NAFASI 06

MAJUKUMU YA KAZI;

  • Kuainisha mahitaji ya mwaka ya dawa na vifaa na kuandaa bajeti yake.
  • Kuagiza, kununua, kuhifadhi na kusambaza dawa na vifaa tiba katika kituo chake cha kazi na kujua mifumo yote ya utumiaji na uagizaji wa dawa zikiwemo na dawa za wapokea huduma waishio na VVU.
  • Kuweka vizuri kumbukumbu za dawa za zana mbalimbali za mifumo ya dawa ikiwemo Pharmacy Module Database.
  • Kuandaa orodha ya dawa za hospitali (Hospital Fomulary) kwa matumizi ya kituo anapofanya kazi zikiwemo dawa za wapokea huduma waishio na VVU
  • Kutoa dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa zikiwemo dawa za wapokea huduma waishio na VVU
    Kusimamia matumizi sahihi ya dawa.
  • Kutengeneza dawa (compounding) kwa matumizi ya kituo anapofanya kazi.
  • Kutoa taarifa juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya dawa (adverse drug reaction).
  • Kuelimisha watumishi walio chini yake, watumishi wengine wa sekta ya Afya na Jamii juu ya matumizi sahihi ya dawa.
  • Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Dawa zikiwemo dawa za wapokea huduma waishio na VVU katika kituo anapofanya kazi.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Awe mwenye Elimu na Cheti cha Kidato cha Nne (IV) waliohitimu mafunzo ya Stashahada katika Fani ya dawa (Pharmacy)kwa miaka mitatu (3) kutoka katika vyuo vinavyotambulika na Serikali
    Awe amesajiliwa na baraza la Famasi.
  • Awe na uzoefu wa kutumia wa Kompyuta hasa program za MS word, excel na powerpoint.
  • Mwenye uzoefu wa kufanya kazi katika vituo vya tiba na matunzo kwa walau mwaka mmoja Vilivyopo Mkoani Geita.
  • Ujuzi wa uchambuzi na utatuzi wa changamoto.
  • Uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha katika Kiingereza na Kiswahili.
  • Uwezo wa kufanya kazi kibinafsi na kama sehemu ya timu yenye usimamizi mdogo.
  • Uwezo wa kudumisha usiri katika nyanja zote

✅AFISA TAKWIMU (DATA OFFICER) – NAFASI 09

MAJUKUMU YA KAZI.

  • Kuingiza takwimu kwa uharaka na usahihi zinazohusu matibabu kwenye CTC2 database.
  • Kuandaa na kufanya mapitio ya takwimu za Afua mbalimbali za VVU/UKIMWI za Kituo kwa wiki, mwezi na Robo.
  • Kufanya upembuzi na kuandaa orodha ya wagonjwa kwa ajili ya ufuatiliaji kama vile wateja waliopotea kwenye huduma, wateja ambao hawajahudhuria kwenye kliniki zao n.k
  • Kuwezesha upembuzi na tafsiri ya takwimu kwa ajili ya kupanga na kufanya maamuzi katika ngazi ya kituo
  • Kutunza kumbukumbu za fomu na mafaili ya wateja kulingana na miongozo
  • Kufanya mlinganyo wa takwimu za Afua za VVU/UKIMWI zilizopo katika vyanzo mbalimbali vya taarifa.

SIFA ZA MWOMBAJI.

  • Awe wenye Elimu na Cheti cha Kidato cha nne (IV) waliohitimu mafunzo ya AStashahada katika Fani ya Takwimu kutoka katika vyuo vinavyotambulika na Serikali na mwenye ujuzi wa kutumia kompyuta.
  • Astashahada, stashahada na zaidi kwa Sayansi ya Kompyuta, Habari za Afya, Takwimu au Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) au fani inayohusiana nayo.
  • Uzoefu usiopungua miaka miwili (2) wa kufanya kazi kama afisa wa uingizaji data katika mipangilio ya programu ya VVU/UKIMWI katika vituo vilivyopo Mkoa wa Geita.
  • Ujuzi wa uchambuzi na utatuzi wa changamoto.
  • Uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha katika Kiingereza na Kiswahili.
  • Uwezo wa kudumisha usiri katika nyanja zote.
  • Uwezo wa kufanya kazi kibinafsi na kama sehemu ya timu yenye usimamizi mdogo.

MASHARTI YA JUMLA

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, nakala za vyeti vya kidato cha nne au cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho.
  • “Testimonials”. “Provisional Results”, “Statements of Results”, hati matokeo za kidato cha nne au cha sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
    Waombaji waliosoma nje ya
  • Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Barua za maombi ya kazi ziandikwe kwa Mkono kuletwa Masjala kwa njia ya Posta au Mkono.

Waambaji wawe wanaojitolea katika vituo vya kutolea Huduma za Afya na barua zao zipitishwe na wafawidhi wa Vituo husika.

Picha moja ya rangi “Passport size” ya hivi karibuni, iandikwe jina kamili la mwombaji.

Barua zote za maombi ziandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

Hakikisha unaandika namba yako ya simu ambayo inapatikana muda wote.

Waombaji ambao ni watumishi wa Umma hawataruhusiwa kuomba nafasi hizi.

Watakaochaguliwa kufanya usaili watajulishwa kwa Tangazo na simu.

Mwisho wa kupokea maombi ya kazi ni tarehe 25.11.2024 saa 09:30 Alasiri.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!