NAFASI 600 ZA WALIMU MDAs & LGAs (PSRS)
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
- Waombaji wa nafasi za Mwalimu Daraja la III B na Mwalimu Daraja la III C wahakikishe wanambatisha HATI YA MATOKEO (ACADEMIC TRANSCRIPT) katika mfumo wa “Ajira Portal” kwa ajii ya utambuzi wa masomo ya kufundishia.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI Computer Certificate Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
POST: MWALIMU DARAJA LA III C – SOMO LA UZALISHAJI WA MAZAO (CROP PRODUCTION) – 20 POST Employer: MDAs & LGAs More Details | 2024-09-30 Login to Apply |
POST: MWALIMU DARAJA LA III B – SOMO LA BIASHARA (COMMERCE) – 125 POST Employer: MDAs & LGAs More Details | 2024-09-30 Login to Apply |
POST: MWALIMU DARAJA LA III C – SOMO LA UVUVI NA USINDIKAJI WA SAMAKI (FISHING AND FISH PROCESSING) – 10 POST Employer: MDAs & LGAs More Details | 2024-09-30 Login to Apply |
POST: MWALIMU DARAJA LA III B – SOMO LA BIASHARA (BOOKKEEPING) – 125 POST Employer: MDAs & LGAs More Details | 2024-09-30 Login to Apply |
POST: MWALIMU DARAJA LA III B – SOMO LA USINDIKAJI WA MBAO (WOOD PROCESSING) – 5 POST Employer: MDAs & LGAs More Details | 2024-09-30 Login to Apply |
